Kitabu cha Mhubiri : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: tl:Eclesiastes
Mstari 95: Mstari 95:
[[ru:Книга Екклесиаста]]
[[ru:Книга Екклесиаста]]
[[simple:Ecclesiastes]]
[[simple:Ecclesiastes]]
[[sr:Књига проповедникова]]
[[sr:Књига Проповедникова]]
[[sv:Predikaren]]
[[sv:Predikaren]]
[[th:ปัญญาจารย์]]
[[th:ปัญญาจารย์]]

Pitio la 22:09, 1 Septemba 2008

Mhubiri ni kitabu cha hekima kilichomo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Ukristo.

Katika lugha ya Kiebrania jina lake ni קֹהֶלֶת (Qohelet), maana yake "Mhadhiri": ndivyo anavyojiita mwandishi.

Yeye anakabili masuala ya maisha kwa kuzingatia upande chanya na upande hasi wa kila moja ili kufikia hekima.

Hasa anajiuliza juu ya maana ya maadili wakati ufunuo wa Mungu ulikuwa haujafikia hatua ya kufundisha uzima wa milele na maisha yalikuwa yanaonyesha mara nyingi ustawi wa waovu na hali ngumu ya waadilifu.

Mbele ya utovu wa haki duniani, Mhubiri alikariri, "Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili" (1:2).

Hata hivyo, hatimaye akajumlisha mawazo yake kwa kuhimiza kwa imani, "Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" (12:13-14).

Maendeleo ya ufunuo yataweka wazi kwamba hukumu hiyo itafanyika baada ya kifo, na kwamba tuzo na adhabu vitatolewa kwa haki katika uzima wa milele.