Tanzania : Tofauti kati ya masahihisho
d robot Adding: az:Tanzaniya |
dNo edit summary |
||
Mstari 32: | Mstari 32: | ||
| [[Wakazi kwa km²]] || 39 |
| [[Wakazi kwa km²]] || 39 |
||
|---- |
|---- |
||
| [[Uhuru]] || kutoka [[Uingereza]] tar. 9 |
| [[Uhuru]] || kutoka [[Uingereza]] tar. [[9 Desemba]], [[1961]] |
||
|---- |
|---- |
||
| [[Pesa]] || [[Shilingi ya Tanzania]] |
| [[Pesa]] || [[Shilingi ya Tanzania]] |
Pitio la 14:54, 6 Septemba 2006
| |||||
Wito: Uhuru na Umoja | |||||
Lugha rasmi | Kiswahili, Kiingereza | ||||
Mji Mkuu | Dodoma | ||||
Makao ya Serikali | Daressalam | ||||
Serikali | Jamhuri | ||||
Rais | Jakaya Kikwete | ||||
Waziri Mkuu | Edward Ngoyai Lowasa | ||||
Eneo | 945.087 km² | ||||
Wakazi | 36.766.356 (Julai 2005) | ||||
Wakazi kwa km² | 39 | ||||
Uhuru | kutoka Uingereza tar. 9 Desemba, 1961 | ||||
Pesa | Shilingi ya Tanzania | ||||
Wakati | UTC+3 | ||||
Dini za wakazi | Ukristo (45%), Uislamu (35%), Dini za jadi (20%) | ||||
Wimbo wa Taifa | Mungu ibariki Afrika | ||||
Tanzania ni nchi katika Afrika ya Mashariki. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi, Rwanda na Uganda upande wa magharibi.
Lugha ya kitaifa ya Tanzania ni Kiswahili pamoja na Kiingereza, kinachotumika katika baadhi ya shughuli za kiserikali na biashara. Lakini lugha rasmi ya shughuli za bungeni pia ya elimu ya msingi ni Kiswahili.
Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Mji mkuu: Dodoma, Makao makuu ya serikali: Dar es Salaam, miji mikubwa mingine: Mbeya, Arusha
Historia
(kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)
Neno "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar pamoja na athira ya jina la kale la "Azania". Nchi hizi mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa koloni za kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Uingereza. Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza na hali ya eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.
Hadi 1964 Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti zikaungana na kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza.
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa,ameendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafisishwa. Tar. 21.12.2005 Jakya Kikwete ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa. Tanzania ni moja ya nchi maskini duniani na ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni yake katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane.
Maungano kati ya Tanganyika na Zanzibar:
Tangu maungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata muundo ifuatayo:
- Nchi inatawaliwa na serikali ya manungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
- Tanganyika au Tanzania barani haina serikali au bunge la pekee
- Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake zinazoratibu mambo yasiyo ya maungano.
Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za manungano:
- Mambo ya nje
- Jeshi
- Polisi
- Mamlaka ya dharura
- Uraia
- Uhamiaji
- Biashara ya nje
- Utumishi wa umma
- Kodi ya mapato, orodha
- Mabandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu
Demografia
Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kunaishi mtu mmoja tu kwenye kilomita moja ya mraba (1/km²) lakini sehemu zenye rotuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba. Zaidi ya asilimia themanini huishi vijijini. Dar es Salaam ni mji mkubwa kabisa wenye watu karibu milioni tatu.
Kuna makabila zaidi ya 120. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wahaya, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wachaga na Wagogo. Makabila mengine kwa mfano yanaitwa Wapare, Wasambaa, Warangi na Wangoni. Idadi kubwa sana ya Watanzania ni Wabantu. Nje ya hao, kuna Waniloti, baadhi yao kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya. Kundi lingine ni Wakushi wanaoishi milimani ya kaskazini ya Tanzania; hao ni makabila ya Wambulu, Wafiome, Waburunge na Wasi. Hatimaye, kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina yao ni Wasandawe na Wahadzabe.
Ingawa kila kabila lina lugha yake, lugha ya taifa ya Tanzania ni Kiswahili ambacho ni lugha mojawapo ya lugha za Kibantu. Hali hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.
Utamaduni
Urithi wa Dunia
Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokelewa katika orodha ya UNESCO ya "urithi wa dunia".
(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)
- 1979 – Hifadhi la Taifa Ngorongoro
- 1981 – Hifadhi la Taifa la Serengeti
- 1981 – Maghofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara
- 1982 – Hifadhi la Taifa Selous
- 1987 – Hifadhi la Taifa Kilimanjaro
- 2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |