Wagadugu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ta:வாகடூகு
d roboti Nyongeza: ka:უაგადუგუ
Mstari 47: Mstari 47:
[[it:Ouagadougou]]
[[it:Ouagadougou]]
[[ja:ワガドゥグー]]
[[ja:ワガドゥグー]]
[[ka:უაგადუგუ]]
[[ko:와가두구]]
[[ko:와가두구]]
[[ksh:Ouagadougou]]
[[ksh:Ouagadougou]]

Pitio la 03:39, 17 Agosti 2008

Barabara katika kitovu cha Wagadugu karibu na uwanja wa Umoja wa Mataifa.

Wagadugu (kwa Kifaransa huandikwa Ouagadougou) ni mji mkuu wa Burkina Faso, na pia mji mkubwa kabisa wa nchi hiyo. Mwaka 2005 idadi ya wakazi ilikuwa milioni 1,2. Mji unakua haraka.

Wagadugu iko katika jimbo la Kadiogo. Kuna ofisi za serikali na viwanda kadhaa vya nguo na vyakula.

Mji ni pia kitovu cha usafiri na mawasiliano. Kuna kiwanja cha kimataifa cha ndege na njia ya reli kwenda Abidjan (Côte d'Ivoire), halafu barabara za kwenda Lome (Togo), Bamako (Mali), Niamey (Niger), Accra (Ghana).

Wagadugu ina chuo kikuu kilichokuwa chuo cha mwanahistoria maarufu Joseph Ki-Zerbo. Tamasha la kimataifa la filamu za Afrika (FESPACO) hufanyiwa Wagadugu.

Meya wa mji ndiye Simon Compaoré aliyechaguliwa mwaka wa 1995.