Toni Morrison : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Adding: bn, de, tr, zh Modifying: eo
Mstari 32: Mstari 32:
[[da:Toni Morrison]]
[[da:Toni Morrison]]
[[de:Toni Morrison]]
[[de:Toni Morrison]]
[[el:Τόνι Μόρρισον]]
[[en:Toni Morrison]]
[[en:Toni Morrison]]
[[eo:Toni Morrison]]
[[eo:Toni Morrison]]

Pitio la 18:15, 25 Agosti 2006

Toni Morrison

Toni Morrison ni mwandishi wa kike nchini Marekani na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya fasihi ya mwaka 1993. Alizaliwa kwa jina la Chloe Anthony Wofford tarehe 18 Februari 1931 huko Lorain, Ohio kama mtoto wa pili wa familia ya Waamerika weusi. Wazazi wake walikuwa wafanyakazi.

Alipenda kusoma vitabu tangu utoto. 1949 akajiunga na chuo kikuu cha Howard (chuo kwa Waamerika weusi katika mji mkuu Washington D.C.) akimaliza kwa BA katika Kiingereza. Wakati ule aliacha jina lake la Chloe akatumia "Toni" kama kifupi cha "Anthony". Mwaka 1955 alipata MA katika chuo kikuu cha Cornell.

Alianza kufundisha fasihi kwenye chuo kikuu cha Texas Kusini mjini Houston, tangu 1957 tena Howard. Aliolewa na Howard Morrison akazaa watoto wawili. Baada ya talaka mwaka 1964 alianza kazi ya uhariri wa vitabu kwa wachapishaji wa Random House. Alihariri vitabu vingi vya waandishi weusi.

Mwaka 1970 alitoa kitabu chake cha kwanza "The Bluest Eye" (Jicho la buluu). Kitabu cha kwanza kilichofaulu kuuzwa vema kilikuwa "Song of Solomon" (Wimbo ya Suleimani) mwaka 1977.

Tangu 1989 amefundisha kama profesa katika chuo kikuu cha Princeton. 1993 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Kati ya riwaya zake ni:

  • The Bluest Eye, 1970
  • Sula, 1973
  • Song of Solomon, 1977
  • Tar Baby, 1981,
  • Beloved, 1987
  • Jazz, 1992
  • Paradise, 1998
  • Love, 2003