Tanzania : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 49: Mstari 49:
'''Tanzania''' ni [[nchi]] katika [[Afrika]] ya Mashariki. Imepakana na [[Uganda]] na [[Kenya]] upande wa Kaskazini, [[Bahari Hindi]] mashariki, [[Msumbiji]], [[Malawi]] na [[Zambia]] upande wa kusini, [[Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia|Kongo]], [[Burundi]], [[Rwanda]] na [[Uganda]] upande wa magharibi.

[[Lugha]] ya kitaifa ya Tanzania ni [[Kiswahili]] pamoja na [[Kiingereza]], kinachotumika katika baadhi ya shughuli za [[Serikali|kiserikali]] na [[biashara]].
[[Lugha]] ya kitaifa ya Tanzania ni [[Kiswahili]] pamoja na [[Kiingereza]], kinachotumika katika baadhi ya shughuli za [[Serikali|kiserikali]] na [[biashara]]. Lakini lugha rasmi ya shughuli za [[Bunge|bungeni]] pia ya elimu ya msingi ni [[Kiswahili]].

Tanzania ni nchi mwanachama wa [[Jumuiya ya Afrika ya Mashariki]].
Lakini lugha rasmi ya shughuli za [[Bunge|bungeni]] pia ya elimu ya msingi ni [[Kiswahili]].

Mji mkuu: [[Dodoma]], Makao makuu ya serikali: [[Dar es Salaam]], miji mikubwa mingine: [[Mbeya]], [[Arusha]]

==Historia==
''(kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za [[Tanganyika]], [[Zanzibar]] na [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]])''
Neno "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya [[Tanganyika|TANganyika]] na [[Zanzibar|ZANzibar]] pamoja na athira ya jina la kale la "[[Azania]]". Nchi hizi mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa koloni za kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya [[nchi lindwa]] kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Uingereza. Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani]] hadi [[Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia]] halafu ikawa chini ya Uingereza na hali ya [[eneo la kudhaminiwa]] kutokana na azimio la [[Shirikisho la Mataifa]] iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.

Mstari 59: Mstari 65:
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili [[Ali Hassan Mwinyi]] iliruhusu mfumo wa [[vyama vingi vya siasa Tanzania]] na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya [[Benki ya Dunia]] na [[Shirika la Fedha Duniani]]. Rais wa awamu ya tatu, [[Benjamin Mkapa]],ameendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafisishwa. Tar. 21.12.2005 [[Kikwete, Jakaya|Jakya Kikwete]] ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa. Tanzania ni moja ya nchi maskini duniani na ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni yake katika mpango wa kusamehe madeni wa [[Kundi la Nchi Nane]].
Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili [[Ali Hassan Mwinyi]] iliruhusu mfumo wa [[vyama vingi vya siasa Tanzania]] na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya [[Benki ya Dunia]] na [[Shirika la Fedha Duniani]]. Rais wa awamu ya tatu, [[Benjamin Mkapa]],ameendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafisishwa. Tar. 21.12.2005 [[Kikwete, Jakaya|Jakya Kikwete]] ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa. Tanzania ni moja ya nchi maskini duniani na ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni yake katika mpango wa kusamehe madeni wa [[Kundi la Nchi Nane]].

Tanzania ni nchi mwanachama wa [[Jumuiya ya Afrika ya Mashariki]].

Mji mkuu: [[Dodoma]], Makao makuu ya serikali: [[Dar es Salaam]], miji mikubwa mingine: [[Mbeya]], [[Arusha]]

==Maungano kati ya Tanganyika na Zanzibar:==
==Maungano kati ya Tanganyika na Zanzibar:==

Pitio la 09:52, 18 Agosti 2006

United Republic of Tanzania (Kiing.)
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
(Kiswahili)
Bendera ya Tanzania Nembo ya Tanzania
Bendera ya Tanzania Nembo ya Tanzania

Wito: Uhuru na Umoja

Lugha rasmi Kiswahili, Kiingereza
Mji Mkuu Dodoma
Makao ya Serikali Daressalam
Serikali Jamhuri
Rais Jakaya Kikwete
Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa
Eneo 945.087 km²
Wakazi 36.766.356 (Julai 2005)
Wakazi kwa km² 39
Uhuru kutoka Uingereza tar. 9.12.1961
Pesa Shilingi ya Tanzania
Wakati UTC+3
Dini za wakazi Ukristo (45%), Uislamu (35%), Dini za jadi (20%)
Wimbo wa Taifa Mungu ibariki Afrika
Tanzania katika Afrika
Ramani ya mikoa ya Tanzania

Tanzania ni nchi katika Afrika ya Mashariki. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi, Rwanda na Uganda upande wa magharibi.

Lugha ya kitaifa ya Tanzania ni Kiswahili pamoja na Kiingereza, kinachotumika katika baadhi ya shughuli za kiserikali na biashara. Lakini lugha rasmi ya shughuli za bungeni pia ya elimu ya msingi ni Kiswahili.

Tanzania ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Mji mkuu: Dodoma, Makao makuu ya serikali: Dar es Salaam, miji mikubwa mingine: Mbeya, Arusha

Historia

(kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani)

Neno "Tanzania" limeundwa kutokana na majina ya TANganyika na ZANzibar pamoja na athira ya jina la kale la "Azania". Nchi hizi mbili zilikuwa zote chini ya utawala wa Uingereza hadi kupata uhuru lakini hazikuwa koloni za kawaida. Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Uingereza. Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza na hali ya eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa iliyoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa.

Hadi 1964 Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti zikaungana na kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza.

Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa,ameendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafisishwa. Tar. 21.12.2005 Jakya Kikwete ameapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa. Tanzania ni moja ya nchi maskini duniani na ambazo zimefanikiwa kufutiwa madeni yake katika mpango wa kusamehe madeni wa Kundi la Nchi Nane.

Maungano kati ya Tanganyika na Zanzibar:

Tangu maungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 Tanzania imefuata muundo ifuatayo:

  • Nchi inatawaliwa na serikali ya manungano ikitekeleza sheria zinazotolewa na bunge la Tanzania.
  • Tanganyika au Tanzania barani haina serikali au bunge la pekee
  • Zanzibar (Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake zinazoratibu mambo yasiyo ya maungano.

Mambo yafuatayo yalikubalika kuwa shughuli za manungano:

  • Mambo ya nje
  • Jeshi
  • Polisi
  • Mamlaka ya dharura
  • Uraia
  • Uhamiaji
  • Biashara ya nje
  • Utumishi wa umma
  • Kodi ya mapato, orodha
  • Mabandari, Usafiri wa anga, Posta na Simu

Demografia

Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kunaishi mtu mmoja tu kwenye kilomita moja ya mraba (1/km²) lakini sehemu zenye rotuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba. Zaidi ya asilimia themanini huishi vijijini. Dar es Salaam ni mji mkubwa kabisa wenye watu karibu milioni tatu.

Kuna makabila zaidi ya 120. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wahaya, Wanyakyusa, Wanyamwezi, Wachaga na Wagogo. Makabila mengine kwa mfano yanaitwa Wapare, Wasambaa, Warangi na Wangoni. Idadi kubwa sana ya Watanzania ni Wabantu. Nje ya hao, kuna Waniloti, baadhi yao kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya. Kundi lingine ni Wakushi wanaoishi milimani ya kaskazini ya Tanzania; hao ni makabila ya Wambulu, Wafiome, Waburunge na Wasi. Hatimaye, kuna vikundi viwili vya Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; majina yao ni Wasandawe na Wahadzabe.

Ingawa kila kabila lina lugha yake, lugha ya taifa ya Tanzania ni Kiswahili ambacho ni lugha mojawapo ya lugha za Kibantu. Hali hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu.

Utamaduni

Urithi wa Dunia

Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokelewa katika orodha ya UNESCO ya "urithi wa dunia".

(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)

Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira