True Jesus Church : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ext, gan, kaa, mdf, sah, srn, szl
d roboti Nyongeza: hif:Isa masih saty girajaghar [r5530]
Mstari 99: Mstari 99:
[[he:הכנסייה האמיתית של ישו]]
[[he:הכנסייה האמיתית של ישו]]
[[hi:ईसा मसीह सत्य गिरजाघर]]
[[hi:ईसा मसीह सत्य गिरजाघर]]
[[hif:Isa masih saty girajaghar]]
[[hr:Prava Crkva Isusova]]
[[hr:Prava Crkva Isusova]]
[[hsb:True Jesus Church]]
[[hsb:True Jesus Church]]

Pitio la 00:39, 9 Juni 2008

Faili:T J C.jpg

True Jesus Church (TJC) ni kanisa dogo lililoanzishwa Uchina mwaka 1917. Asili yake ni katika mwelekeo wa Kipentekoste ndani ya Ukristo.

Inadaiwa ya kwamba TJC lina Wakristo milioni 1.5 katika nchi 45. Idadi kubwa wako ndani ya Uchina ambako si rahisi kuhakikisha idadi kamili kwa sababu TSC ni kati ya makanisa na vikundi vya kikristo vilivyopigwa marufuku na serikali ya nchi hiyo. Tovuti za TJC katika nchi mbalimbali zinataja Wakristo mnamo 70,000 hadi 80,000 katika "nchi huru", wengi wao wakiwa na asili ya Kichina. Tangu mwaka 2002 TJC lilianza kuwasiliana na kikundi cha kikristo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilichojiunga nalo mnamo mwaka 2004.

TJC linashika imani mbalimbali za pekee zinazotofautisha kikundi hiki na makanisa mengine ya Kikristo. Kimsingi wanaamini ya kwamba wenyewe ni kanisa pekee la kweli la Kristo; makanisa mengine yote ni ya uwongo. Wanajieleza kwamba Kristo alianzisha Kanisa moja la kimitume lililopeleka Injili katika nchi mbalimbali. Lakini Kanisa hilo likavurugika na kupatwa imani potovu na uzushi. Mwaka 1917 Mungu aliamua kulifufua Kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu na ndio mwanzo wa TJC.

Kati ya imani nyingine za pekee ni hizi zifuatazo:

  • atakayebatizwa lazima akubali TJC ni mwili wa Kristo.
  • Wakataza mafundisho ya Utatu wa Mungu wakisema "Yesu yu Mungu wa kweli".
  • Wanakataza ibada za Jumapili wakidai siku ya Jumamosi ndiyo siku takatifu ya Sabato iliyoamriwa na Mungu.
  • Hawasheherekei sikukuu za Krismasi na Pasaka kwa sababu wanaamini zina asili za kipagani na ni mifano ya imani ya Kikristo ya asili kuingiliwa na uzushi.
  • Wanaangalia desturi ya kuosha miguu kama sakramenti iliyoamriwa na Yesu Kristo.

Mafundisho mengine yanafanana na yale ya Wapentekoste wengine, kama vile kusema kwa lugha za roho au kubatizwa kwa jina la Yesu kwa kuzamisha chini ya maji, tena maji ya kutiririka.

TJC ni kati ya vikundi vinavyojitahidi sana kusambaza habari zao kupitia tovuti. Tangu 2005 hadi Aprili ya mwaka 2006 wamefaulu kuingiza habari zao katika Wikipedia za lugha 114 lakini mara nyingi makala hizo ni tafsiri tu ya maelezo waliyoyaandaa wenyewe. Ingefaa yajadiliwe na watu wengine. Kwa mfano, ingefaa ieleweke ukweli wa msimamo wa TJC kulingana na Biblia wanapodai kwa miaka mia kadhaa duniani halikuwepo tena Kanisa la kweli. Mbona Yesu aliahidi, "Nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20)? Tena "Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda" (Mathaio 16:18). ak:Ỳesu Asafo Ankasaankasa