Barack Obama : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 50: Mstari 50:
[[fr:Barack Obama]]
[[fr:Barack Obama]]
[[ga:Barack Obama]]
[[ga:Barack Obama]]
[[gan:奧巴馬]]
[[gl:Barack Obama]]
[[gl:Barack Obama]]
[[gv:Barack Obama]]
[[gv:Barack Obama]]
Mstari 66: Mstari 67:
[[ksh:Barack Obama]]
[[ksh:Barack Obama]]
[[ku:Barack Obama]]
[[ku:Barack Obama]]
[[la:Barack Obama]]
[[la:Baracus Obama]]
[[lb:Barack Obama]]
[[lb:Barack Obama]]
[[lt:Barack Obama]]
[[lt:Barack Obama]]
Mstari 91: Mstari 92:
[[tr:Barack Obama]]
[[tr:Barack Obama]]
[[uk:Обама Барак]]
[[uk:Обама Барак]]
[[ur:بارک اوبامہ]]
[[vi:Barack Obama]]
[[vi:Barack Obama]]
[[vls:Barack Obama]]
[[vls:Barack Obama]]

Pitio la 10:57, 8 Juni 2008

Seneta Barack Obama

Barack Hussein Obama (* 4 Agosti 1961) ni mwanasiasa nchini Marekani na tangu 2004 yeye ni seneta wa jimbo la Illinois katika bunge la kitaifa. Tangu mwaka 2007 ametafuta nafasi ya mgombea wa chama cha Demokrasia (Democratic Party) kwa uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008.

Alipoingia bungeni alikuwa seneta wa kitaifa wa pekee Mwamerika mweusi.

Utoto na Ujana

Baba yake Obama alikuwa Mkenya Barack Obama aliyeaga dunia 1982. Mzee Obama alitoka mkoa wa Nyanza nchini Kenya akaenda Marekani masomoni. Mama yake, Ann Dunham, alikuwa Mwamerika mzungu kutoka jimbo la Kansas aliyeaga dunia 1995. Wazazi walifunga ndoa wakati ndoa kati ya watu weupe na weusi bado ilikuwa marufuku katika sehemu za kusini za Marekani. Wazazi waliachana baada ya miaka miwili na mtoto Barack alibaki na mama.

Baadaye mama yake aliolewa na mwanafunzi kutoka Indonesia akamfuata aliporudi kwake. Hivyo Barack aliishi Jakarta hadi 1971 aliporudi Marekani na kukaa na babu yake huko Hawaii hadi alipomaliza shule ya sekondari.

Barack ana dada wawili, mmoja kutoka ndoa ya pili ya mama yake na mmoja kutoka ndoa ya pili ya baba yake huko Kenya.

Masomo na kazi

Baada ya kumaliza sekondari alisoma siasa na sheria katika vyuo vya Occidental huko Los Angeles]], Columbia huko New York na Harvard. 1991 alimaliza kwa digrii ya dokta.

Baada ya digrii ya kwanza Obama aliwahi kufanya kazi ya kijamii huko Chicago. 1991 alirudi Chicago alipopata kazi katika ofisi ya wanasheria akafundisha pia kozi za sheria kwenye chuo kikuu cha Chicago.

Kuingia katika siasa

1996 alichaguliwa kama seneta wa bunge la Illinois akarudishwa 1998 na 2002. 2004 alichaguliwa kuwa seneta wa bunge la kitaifa.

Familia

Obama alimwoa Michelle Robinson ambaye ni mwanasheria kama yeye mwenyewe. Wana mabinti wawili. Familia ina nyumba yake huko Chicago.

Viungo vya Nje