Mbeya (mji) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: no:Mbeya
d roboti Nyongeza: it:Mbeya
Mstari 40: Mstari 40:
[[eo:Mbeya]]
[[eo:Mbeya]]
[[fr:Mbeya]]
[[fr:Mbeya]]
[[it:Mbeya]]
[[no:Mbeya]]
[[no:Mbeya]]
[[pl:Mbeya (miasto)]]
[[pl:Mbeya (miasto)]]

Pitio la 16:41, 6 Juni 2008

Faili:Mbeya Loleza.jpg
Mlima wa Loleza juu ya mji wa Mbeya

Mji wa Mbeya ni mji mkubwa katika kusini-magharibi ya Tanzania. Mbeya ni kitovu katika Nyanda za Juu za Kusini ambazo ni eneo la uzalishaji wa mazao mengi. Ni makao makuu ya mkoa na wilaya.

Jiografia

Mji umeenea katika bonde kati ya safu za milima ya Mbeya na milima ya Uporoto. Mlima mkubwa unaoonekana kutoka mji ni Mlima wa Mbeya (Mbeya Peak) mwenye kimo cha 2818 m. Eneo la mji ni kati ya 1600 m kitovuni na 1900 m au zaidi juu ya UB kwenye mitelemko ya mlima Loleza.

Hali ya hewa haina joto kali kutokana na kimo. Wakati wa Juni-Julai halijoto wakati wa usiku inaweza kushuka chini hadi 0 °C, mlimani hata chini zaidi. Mvua zinaanza mwezi wa Novemba hivyo ni wakati wa kupanda. Kwa kawaida mvua zinasimama tena Januari - Februari na kunyesha kwa wingi Machi -April.

Mawasiliano

Mbeya ni njiapanda ya njia mbalimbali muhimu: Barabara kuu ya lami kutoka Daressalaam (850 km) hugawanya hapa kwenda MalawiMsumbiji kupitia Tukuyu/Rungwe, na kwenda ZambiaAfrika Kusini kupitia Tunduma/Mbozi. Vilevile njia ya reli ya TAZARA hupita Mbeya kuelekea Zambia. Kuna ghala kubwa kwa ajili ya mizigo ya Malawi inayofikishwa kwa reli kutoka Daresalaam bandarini ikihamishwa kwa malori kwenda Malawi hapa Mbeya.

Mbeya imekuwa na uwanja wa ndege mdogo usiokuwa na huduma ya kawaida kwa muda mrefu. Lakini kuna mipango ya kujenga uwanja mpya huko Songwe zipatao km 40 kufuata njia ya kwenda Zambia.

Wakazi

Mbeya ni kati ya miji kumi mikubwa ya Tanzania. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa wapatao 280.000 katika mw. 2005. Wengine mnamo 300.000 wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wsafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwena Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

Uchumi

Uchumi wa Mbeya mjini umetegemea kilimo cha mazingira yake na biashara. Viwanda mbalimbali vilianzishwa lakini havikufaulu sana. Kuna viwanda kwa mfano Zana za Kilimo, Highland Soap, Mbeya Textiles. Mbeya Ceramics iliporomoka kitambo.

Tangu miaka ya 1990 kitovu cha mji kinahamishwa kutoka eneo la zamani kwenda karibu na barabara kuu ya Daresalaam – Zambia.


Historia

Mbeya imeanzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927 wakati dhahabu ilipopatikana mlimani. Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa "Ibheya" ambayo maana yake ni chumvi. Hivyo ba si kwenye miaka ya awali wafanya biashara walikuwa wanafika mahali hapo kubadilishana mazao yao kwa chumvi. Sehemu kubwa ya wakazi ni wakristo, hasa wafuasi wa Kanisa la Katoliki, Kanisa la Moravian, Kanisa la Kiluteri. Kuna pia msikiti kubwa na hekalu ya Wahindu.

Elimu

Pamoja na shule za sekondari kuna taasisi kadhaa za elimu ya juu kama vile:

  • Chuo Kikuu Teofilo Kisanji ambacho ni chuo kikuu changa cha Kanisa la Moravian Tanzania kinachotoa kozi za ualimu na tholojia tangu mwaka 2005. Kilitanguliwa na chuo cha Motheco.
  • Mbeya Technical College
  • Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole) ambacho ni taasisi ya uchunguzi wa kisayansi pamoja na chuo.