Wole Soyinka : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 16: Mstari 16:
Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide akazaa naye watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.
Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide akazaa naye watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.

==Viungo vya nje==
*[http://www.wolesoyinka.blogspot.com Wole Soyinka. All you want to know about.]





Pitio la 16:09, 10 Agosti 2006

Faili:Soyinka.jpg
Wole Soyinka

Akinwande Oluwole au "Wole" Soyinka ni mwandishi Mnigeria na mshindi Mwafrika wa kwanza wa Tuzo ya Nobel ya fasihi (mwaka wa 1986). Wengi wanamwona ndiye mwandishi bora wa michezo ya kuigiziwa Afrika.

Alizaliwa tar. Julai 13, 1934 kwa wazazi Wayoruba huko Abeokuta, Nigeria. Alisoma shule ya msingi kwao Abeokuta halafu shule ya sekondari ya Ibadan. Alifuata masomo ya fasihi Chuo Kikuu huko Ibadan (1952-1954) na Leeds (Uingereza) 1954-1957.

Alifundisha fasihi kwenye vyuo vikuu vya Lagos, Ibadan, na Ife.

Soyinka aligongana mara nyingi na serikali za kidikteta za nchi yake akipinga pia udikteta katika nchi mbalimbali kama vile utawala wa Mugabe huko Zimbabwe.

Katika maandishi yake alilenga mara nyingi kwa "buti inayokandamiza bila kujali rangi ya mguu ndani yake". Hasa wakati wa udikteta wa jenerali Sani Abacha (1993-1998) Soyinka alijikuta hatarini. Akaondoka Nigeria akaishi nje alipopata nafasi ya profesa ya fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Emory (Atlanta - Marekani).

Baada ya mwisho wa utawala wa kijeshi mwaka 1999 Soyinka alikubali nafasi kwenye chuo kikuu cha Ife kwa masharti ya kwamba mwanajeshi mstaafu hatakuwa kamwe chansela wa chuo kikuu kile.

Mwaka 2005 Soyinka ni profesa kwenye chuo kikuu cha Nevada, Marekani.

Wole Soyinka amemwoa mke wake Laide akazaa naye watoto wanne. Aliwahi kuwa na watoto wawili kabla ya kuoa.

Viungo vya nje