Emma Goldman : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
'''Emma Goldman''' (27 Juni, 186914 Mei, 1940) alikuwa akifahamika zaidi kama mtawala huria wa mwshoni mwa miaka ya 1800 hadi katikati mwa miaka ya 1900....
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:52, 15 Mei 2008

Emma Goldman kunako mwaka wa 1910.

Emma Goldman (27 Juni, 186914 Mei, 1940) alikuwa akifahamika zaidi kama mtawala huria wa mwshoni mwa miaka ya 1800 hadi katikati mwa miaka ya 1900.

Imani

Emma Goldman alikuwa mtawala huria(utawala huria ni nadharia ya siasa inayo sema siasa na sheria havitikiwi), hivyo hakuwa anapenda serikali. Alifahamika sana kwa mcommunist-huria kwasababu pia nayeye alikuwa na fikra za kikommunisti.

Aliamini kwamba kwamba watu wanapaswa wawe na maisha yao wenyewe, hivyo kila mtu atakuwa sawa na mwenziwe. Pia alikuwa mstari wa mbele katika kutaka haki sawa kwa wakinamama na alikuwa mtu wa kwanza kulilia haki za mashoga. Goldman pia alikuwa Mkanaji Mungu.

Goldman alikuwa akitetea sana mambo ya kutumia ubavu kwa ya imani ya kuleta mapinduzi halisi katika jamii, lakini baadaye alibadilisha kauli hiyo na kudai kwamba ubavu utatumikia katika kujilinda mwenyewe na si vinginevyo.

Maisha yake

Historia

Goldman alizaliwa katika mji wa Lithuania ya leo (wakati ilikuwa moja kati ya sehemu ya Urusi). Alivyofikisha umri wa miaka kumi na misaba akahamia mjini Rochester, New York akiwa pamoja na dada yake.

Mwanzo kabia alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kutengeneza nguo na akabahatika kuolewa na mfanyakazi mwenziye Bw. Jacob Kersner. Lakini ndoa yao haikudumu sana na Bi. Emma akaelekea zake mjini New York ambako huko ndiko aliko kuja kuwa mmoja wa watawala huria.

Akaja kuwa rafiki mkubwa wa Bw. Alexander Berkman (mtawala huria mwenzi) na akamsaidia kupanga mpango wa kumwua Bw. Henry Clay Frick, tajiri anayesemekana kuwanyanyasa wafanyakazi wake. Lakini Bw. Berkman hakufanikiwa katika mpango huo badala yake akatumikia kifungo cha miaka kumi na minne jela, lakini Goldman hakupatiwa adhabu yoyote ile.

Goldman amekumbana na matatizo kinao ya kisheria. Mnamo mwaka wa 1893, alihukumiwa kwa kosa la kuanzisha mzozo na akatumikia mwaka mmoja jela. Kunako mwaka wa 1901, Emma alitiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusishwa na njama za kuawa kwa rais wa 25 wa Marekani Bw. William McKinley, lakini akakutanika kuwa hana kosa na tuhuma hizo.

Mnamo kwa wa 1916 alitumikia kifungo jela kwa kosa la kutoa taarifa za siri za sehemu ya kuzalishia watu (ambapo kwa kipindi ilikuwa ikihesabia kuwa kama kosa la jinai). Mnamo mwaka wa 1917 alikamatwa na kutiwa ndani kwa kosa la kuto kubaliana na swala la kuanzisha Vita ya Kwanza ya Dunia.

Mnamo mwaka wa 1919, Goldman na Berkman walifukuzwa nchini Mareakani, na kurudi kwao Urusi kwasababu serikali ya Marekani ilikuwa ikiwafikiria kuwa watu hao ni hatari sana kwa taifa lao hivyo warudishwe makwao haraka iwezekanvyo. Baada ya kurudi huko, na Mapinduzi ya Urusi yakawa yashatokea, hivyo Goldman akawa na imani kwamba sasa Urusi huenda ikawa sehemu nzuri.

Matokeo yake akawa anadai kwamba mapinduzi Urusi hayakuwa mazuri kama vile alivyokuwa akifikiria na kusema kwamba Bw. Bolsheviks anawafanyia danganyatoto watu wengi wa nchini Urusi. Alifikira kwamba Bolsheviks alikuwa mtu wa kupenda kudhibiti watu na mwenyewe nguvu zaidi. Pia aliuchukia sana Umoja wa Kisovyeti kwa kuwaweka ndani Wanaharakati wenzake wa utawala huria kwa kosa la kuto kubaliana na watu hao wanaojiita wanautawala huria.

Emma na Berkman waliondoka nchini Urusi baada ya miaka miwili na Goldman akawa anaishi katika sehemu nyingi za nchi za Ulaya, ikiwemo Uingereza na Ufaransa. Mnamo mwaka wa 1936 alielekea zake nchini Hispania kwenda kuwasaidia wanautawala huria wenzi dhidi ya utawala wa kimabavu wakati ule wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispani.

Emma alifariki dunia mnamo tarehe 14 ya mwezi wa Mei katika mwaka wa 1940, kwa ugonjwa wa kupooza. Na kuzikwa karibu kidogo na mji wa Chicago.

Viungo vya nje