Tungamo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Tags: KihaririOneshi Mobile edit Mobile web edit
Mstari 1: Mstari 1:
'''Masi''' (kutoka [[Kiingereza]]: "mass"; kwa [[Kiswahili]] pia: '''Tungamo''') katika [[elimu]] ya [[fizikia]] ni [[tabia]] ya [[mata]], na kwa njia hii pia tabia ya [[gimba]] au [[dutu]].
'''Masi''' (kutoka [[Kiingereza]]: "mass"; kwa [[Kiswahili]] pia: '''Tungamo''') katika [[elimu]] ya [[fizikia]] ni [[tabia]] ya [[mata|maada]], na kwa njia hii pia tabia ya [[gimba]] au [[dutu]].


[[Kipimo sanifu cha kimataifa]] cha masi ni [[kilogramu]]. [[Alama]] yake katika [[fomula]] kwa kawaida ni <math>m</math>.
[[Kipimo sanifu cha kimataifa]] cha masi ni [[kilogramu]]. [[Alama]] yake katika [[fomula]] kwa kawaida ni <math>m</math>.

Pitio la 14:31, 27 Mei 2022

Masi (kutoka Kiingereza: "mass"; kwa Kiswahili pia: Tungamo) katika elimu ya fizikia ni tabia ya maada, na kwa njia hii pia tabia ya gimba au dutu.

Kipimo sanifu cha kimataifa cha masi ni kilogramu. Alama yake katika fomula kwa kawaida ni .

Masi na uzani

Masi ni tofauti na uzani lakini katika maisha ya kawaida hatuoni tofauti. Hivyo tunatumia kipimo cha kilogramu pia kwa kutaja uzani wa sukari tunayonunua. Lakini hali halisi uzani wa gimba au masi ileile ni tofauti kutegemeana na graviti mahali ilipo. Kwa mfano mtu akifika juu ya mwezi uzani ni sehemu ya sita ya uzani wake duniani. Kwa hiyo mtu mwenye uzito wa kilogramu 60 duniani atakuwa na kilogramu 10 pekee akipimwa juu ya mwezi. Sababu yake ni ya kwamba graviti ya mwezi ni ndogo kuliko duniani.

Masi na graviti

Graviti ya gimba fulani inategemeana na masi yake. Kila kitu hata gimba dogo kama jiwe, meza au mtu lina graviti yake. Ila tu masi kubwa ya dunia yetu inafanya graviti yake yaani nguvu inayosababisha ya kwamba watu na vitu havielei hewani bali kukaa kwenye uso wa ardhi tukivutwa kuelekea kitovu cha sayari yetu. Vitu vyote vinavyoshikwa na graviti ya dunia vina graviti yao vilevile lakini kwa sababu masi ya watu na vitu ni ndogo kabisa kuliko masi ya dunia hatuwezi kusikia tofauti. Pia mwezi unavutwa na graviti ya dunia yetu lakini masi ya mwezi ni kubwa kiasi kwamba graviti ya mwezi inaathiri pia dunia. Hii inaonekana kirahisi kutokana na mabadiliko ya bahari kuwa maji kujaa na kupwa yanayosababishwa na uvutano wa graviti ya mwezi.

Masi na inesha

Masi inafanya pia inesha (inertia) ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya masi kubaki katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje. Masi kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kwa urahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: masi zake ni tofauti, hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tungamo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.