Charles Sacleux : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 12: Mstari 12:


==Viungo vya Nje==
==Viungo vya Nje==
*[[http://nn.wikipedia.org/wiki/Brukar:Dittaeva/Afrikastudier/Modul_C/stubbar_fr%C3%A5_pensum Amidu kuhusu Sacleux]]
*[http://nn.wikipedia.org/wiki/Brukar:Dittaeva/Afrikastudier/Modul_C/stubbar_fr%C3%A5_pensum Amidu kuhusu Sacleux]
*[[http://www.missie-geest.nl/Bagamoyo.htm Kazi ya Sacleux huko Bagamoyo]]
*[[http://www.missie-geest.nl/Bagamoyo.htm Kazi ya Sacleux huko Bagamoyo]]



Pitio la 06:07, 27 Machi 2008

Charles Joseph Sacleux (1856–1943) alikuwa padre na misionari kutoka Ufaransa aliyekaa miaka mingi Afrika ya Mashariki hasa Bagamoyo. Anakumbukwa kwa utaalamu wake wa lugha na pia utafiti wake juu ya mimea ya Afrika.

Sacleux alikuwa padre wa shirika ya Roho Mtakatifu.

Sacleux alikuwa misionari mkatoliki wa kwanza aliyeandika juu ya Kiswahili. Alitunga sarufi na kamusi ya Kiswahili. Mwaka 1891 alitunga kamusi ya "Dictionnaire Français—Swahili" iliyochapishwa 1941. Mwaka 1909 alitoa "Grammaire des dialectes Swahilis" (sarufi ya lahaja za Kiswahili). Vitabu vyote viwili vilisifiwa na wataalamu.

Alitunga na kutafsiri vitabu kwa Kiswahili akaandika nyimbo za kiroho zinazotumiwa hadi leo katika kanisa katoliki.

Alitunga pia kamusi ya Kiswahili cha Komori "Le dictionnaire Comorien-Francais et Francais-Comorien".

Katika kazi yake ya botania alikusanya mimea mingi ya Afrika ya Mashariki na kuieleza akapokea tuzo za kitaalamu kwa utafiti huu.

Viungo vya Nje