Zodiaki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Replacing Ophiuchus_zodiac.svg with File:Ophiuchus.svg (by CommonsDelinker because: File renamed: per other signs).
Mstari 82: Mstari 82:
| [[Hawaa (kundinyota)|Hawaa]]
| [[Hawaa (kundinyota)|Hawaa]]
| Ophiuchus
| Ophiuchus
| [[File:Ophiuchus zodiac.svg|50x25px|Hawaa]]
| [[File:Ophiuchus.svg|50x25px|Hawaa]]
| 247,7°–266,3°
| 247,7°–266,3°
| 30 Nov – 18 Des
| 30 Nov – 18 Des

Pitio la 12:07, 30 Novemba 2021

Zodiaki angani, mchoro wa mwaka 1442 katika kuba ya kanisa la Italia, ikionyesha mstari wa njia ya Jua kati ya makundinyota ya ekliptiki.

Zodiaki ni kanda kwenye anga zenye upana wa takriban nyuzi 20 zinazofuata mstari wa ekliptiki yaani mstari wa njia dhahiri ya Jua angani katika mwendo wa mwaka mmoja. Mstari huo unapatikana kwa kutazama Jua wakati wa mapambazuko ambako linaonekana katika mazingira ya makundinyota tofauti. Kila mwaka Jua linapambazuka katika eneo la makundinyota yaleyale.

Njia dhahiri za Mwezi na sayari zinaonekana pia katika kanda hii ya zodiaki.

Hadi leo unajimu unatumia makundinyota 12 kama buruji za falaki kwa imani ya kwamba nyota hizi zina athari kwa kipindi fulani cha mwaka kinachoitwa kufuatana na kundinyota au buruji ya falaki yake. Lakini hali halisi Jua linapita katika maeneo ya makundinyota 13, si 12.

Miaka 3000 iliyopita, ambapo mfumo wa Zodiaki ulibuniwa, wataalamu wa Babeli waliondoa kundinyota la Hawaa (Ophiuchus) katika mfumo kwa shabaha ya kupata mgawanyo wa anga unaolingana na miezi 12 ya kalenda.

Kumetokea pia badiliko la kwamba makundinyota ya Zodiaki hayalingani tena na vipindi vya mwaka ambapo yanatangazwa na wanajimu wa leo. Sababu yake ni kusogea kwa mhimili wa Dunia na hii inasababisha ya kwamba sisi tunatazama anga kwa pembe tofauti kuliko wazee miaka 2000 iliyopita. Ila tu wanajimu wanaendelea kutumia vipindi vilivyopimwa zamani zile.

Makundinyota ya ekliptiki

Jedwali lifuatalo linaonyesha hali halisi ya makundinyota 13 yanayopitiwa na Jua katika mwendo wa mwaka mmoja. Kwa sasa nukta ya machipuo iko ndani ya Hutu (Pisces) hivyo hapa iko nafasi ya 0°

Kundinyota Ishara Nafasi kwenye
ekliptiki
Kipindi cha kupita
kwa Jua (mwaka 2010)
Kipindi cha Buruji ya Falaki
inayolingana katika unajimu
Kiswahili Kilatini
Kondoo (Hamali) Aries Hamali 28,8°–53,5° 19. Apr – 14. Mei 21 Machi- 19 Aprili
Ng'ombe (Tauri) Taurus Thauri 53,5°–90,2° 14 Mei – 21 Juni 20 Aprili – 21 Mei
Mapacha (Jauza) Gemini Jauza 90,2°–118,1° 21 Juni– 20. Julai 22 Mei – 20 Juni
Kaa (Saratani) Cancer Saratani 118,1°–138,2° 20 Julai – 11. Agosti 21 Juni – 22 Julai
Simba (Asadi) Leo Löwe 138,2°–173,9° 11 Agosti – 17. Sept 23 Julai – 22 Agosti
Mashuke (Nadhifa) Virgo Nadhifa 173,9°–218,0° 17 Sept – 31 Okt 23 Agosti – 22 Sept
Mizani Libra Mizani 218,0°–241,0° 31 Okt – 23 Nov 23 Sept – 23 Okt
Nge (Akarabu) Scorpius Akarabu 241,0°–247,7° 23 Nov – 30 Nov 24 Okt – 21 Nov
Hawaa Ophiuchus Hawaa 247,7°–266,3° 30 Nov – 18 Des (ilipunguzwa katika unajimu)
Mshale (Kaus) Sagittarius Kausi 266,3°–299,7° 18 Des – 20 Jan 22 Nov – 21 Des
Mbuzi (Jadi) Capricornus Jadi (Capricornus) 299,7°–327,6° 20 Jan – 16 Feb 22 Des – 19 Jan
Ndoo (Dalu) Aquarius Dalu (Aquarius) 327,6°–351,6° 16 Feb – 12 Machi 20 Jan – 18 Feb
Samaki (Hutu) Pisces Hutu (Pisces) 351,6°–28,8° 12 Machi – 19 Apr 19 Feb – 20 Machi

Tazama pia

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano