Bastola : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
 
No edit summary
Mstari 7: Mstari 7:
Kiasili bastola ilikuwa tu umbo dogo la [[gobori]]. Baada ya kila pigo ilihitaji kujazwa upya.
Kiasili bastola ilikuwa tu umbo dogo la [[gobori]]. Baada ya kila pigo ilihitaji kujazwa upya.

Kwa muda bastola zenye kasiba mbili au zaidi zilitengenezwa kwa kusidi la kuongeza kasi ya kufyatulia risasi.
Kwa muda bastola zenye kasiba mbili au zaidi zilitengenezwa kwa kusudi la kuongeza kasi ya kufyatulia risasi.

Baada ya kupatikana kwa ramia za metali katika karne ya 19 bastola ilipewa chemba ya risasi inayozunguka. Modeli mashuhuri ya mwanzoni ilikuwa aina ya Colt. Kwa kiingereza aina hii huitwa "revolver" kutokana na mzunguko wa chemba. Chemba huwa na ramia 5-8 mara nyingi ni sita.

Pitio la 09:51, 18 Machi 2008

Bastola aina za revolver
Faili:Pistol Browning SFS.jpg
Bastola ya Browning ina chemba ya kubadilisha

Bastola ni silaha ya moto ndogo yenye kasiba fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja tu. Teknolijia yake ni karibu sawa na bunduki isipokuwa ni ndogo.

Aina za bastola

Kiasili bastola ilikuwa tu umbo dogo la gobori. Baada ya kila pigo ilihitaji kujazwa upya.

Kwa muda bastola zenye kasiba mbili au zaidi zilitengenezwa kwa kusudi la kuongeza kasi ya kufyatulia risasi.

Baada ya kupatikana kwa ramia za metali katika karne ya 19 bastola ilipewa chemba ya risasi inayozunguka. Modeli mashuhuri ya mwanzoni ilikuwa aina ya Colt. Kwa kiingereza aina hii huitwa "revolver" kutokana na mzunguko wa chemba. Chemba huwa na ramia 5-8 mara nyingi ni sita.

Aina ya pili kati ya bastola ina chemba ya risasi kama dawati ndogo inayosukumwa ndani ya nafasi yake kwenye bastola. Wanajeshi waliona faida ya kwamba ni rahisi kujaza chemba ya ziada na kuibeba kama akiba inayobadilishwa haraka kuliko kujaza upya chemba inayozunguka kwa sababu chemba ya kuzunguka haitolewi ni lazima kuijaza ramia moja-moja.

Matumizi ya bastola na bunduki

Faida yake kulingana na bunduki yenyewe ni nyepesi na ndogo hivyo haisumbui wakati wa kubeba. Hasara yake katika ulinganisho na bunduki ni hasa mfiko mdogo, nguvu ya risasi zake na umakinifu wa kulenga.

Jeshini bastola hutumiwa kama silaha ya pili pamoja na bunduki. Kwa polisi huwa ni silaha kali ya kawaida. Majambazi mara nyingi hupendelea bastola kwa sababu zinafichwa rahisi hazionekani.