Namba za Flamsteed : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
#WPWP #WPWPARK
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha: Atlas_Coelestis-1.jpg|thumb| Namba za Flamsteed]]

'''Namba za Flamsteed''' (ing. ''[[:en:Flamsteed designation|Flamsteed designation]]'') ni utaratibu wa kutaja nyota uliobuniwa na Mwingereza [[John Flamsteed]] aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa [[paoneaanga]] pa [[Greenwich]] (''[[:en:Royal Greenwich Observatory|Royal Greenwich Observatory]]'').
'''Namba za Flamsteed''' (ing. ''[[:en:Flamsteed designation|Flamsteed designation]]'') ni utaratibu wa kutaja nyota uliobuniwa na Mwingereza [[John Flamsteed]] aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa [[paoneaanga]] pa [[Greenwich]] (''[[:en:Royal Greenwich Observatory|Royal Greenwich Observatory]]'').



Pitio la 11:42, 23 Julai 2021

Namba za Flamsteed

Namba za Flamsteed (ing. Flamsteed designation) ni utaratibu wa kutaja nyota uliobuniwa na Mwingereza John Flamsteed aliyekuwa mkurugenzi wa kwanza wa paoneaanga pa Greenwich (Royal Greenwich Observatory).

Katika orodha yake nyota zinatajwa kwa namba na kundinyota. Kwa njia hii aliweza kutaja kwa namna ya pekee karibu kila nyota inayoonekana kwa macho matupu.

Mfumo wa Flamsteed unafanana na mfumo wa Bayer aliyetumia jina la kundinyota pamoja na herufi za Kigiriki kwa mfano Alfa Centauri akipata matatizo katika makundinyota makubwa ambayo idadi ya nyota inazidi idadi ya herufi za Kigiriki. Hapo mfumo wa Flamsteed haukuwa na mipaka kutaja hata nyota nyingi.

Flamsteed alitumia uhusika milikishi (en:genitive) wa jina la Kilatini ya kundinyota akiongeza namba (Mfano: Centaurus - uhusika milikishi "Centauri").

Siku hizi namba za Flamsteed zinatumiwa pamoja na majina ya Bayer hasa pale ambako zinahusu nyota ambazo Bayer hakutolea majina, kwa mfano kwa sababu Bayer aliorodhesha 1,564 nyota pekee zinazoonekana kwa macho matupu ilhali Flamsteed alitumia darubini na hivyo aliorodhesha nyota 2,554. Mara nyingi namba za Flamstee zimekuwa kawaida pale ambako Bayer alilazimishwa kuongeza herufi za Kilatini au namba kwa zile za Kigiriki kutokana na idadi ya nyota katika kundinyota fulani. Kwa mfano namba ya Flamsteed "55 Cancri" hupendelewa na jina la Bayer "Rho-1 Cancri".

Marejeo

Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano


http://galileo.rice.edu/Catalog/NewFiles/flamsted.html