Mfalme : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d wikidata interwiki
dNo edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Image:Forms of government.svg|thumb|450px|'''Aina za serikali duniani'''
aina za [[Jamhuri]]: buluu, kijani, njano na machungwa;
'''[[Ufalme]]''':
'''nyekundu''' Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka madogo tu ya kisiasa
'''dhambarau''':Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka makubwa
'''dhambarau nyeusi''': mfalme ana madaraka yote habanwi na katiba
'''Mengine''': Utawala wa chama kimoja au kamati ya kijeshi]]
[[Image:Forms of government 2021.svg|thumb|450px|'''Aina za serikali duniani'''
aina za [[Jamhuri]]: buluu, kijani, njano na machungwa;
'''[[Ufalme]]''':
'''nyekundu''' Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka madogo tu ya kisiasa
'''dhambarau''':Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka makubwa
'''dhambarau nyeusi''': mfalme ana madaraka yote habanwi na katiba
'''Mengine''': Utawala wa chama kimoja au kamati ya kijeshi]]

'''Mfalme''' ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa [[ufalme]]. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.
'''Mfalme''' ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa [[ufalme]]. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Pitio la 18:05, 27 Juni 2021

Aina za serikali duniani
aina za Jamhuri: buluu, kijani, njano na machungwa;
Ufalme:
nyekundu Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka madogo tu ya kisiasa
dhambarau:Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka makubwa
dhambarau nyeusi: mfalme ana madaraka yote habanwi na katiba
Mengine: Utawala wa chama kimoja au kamati ya kijeshi

Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu.

Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia".

Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hii huitwa nasaba.

Madaraka ya mfalme

Madaraka ya wafalme walitofautiana kati ya nchi na nchi na kati ya kipindi na kipindi cha historia. Mifano ni:

• Mfalme wa kikatiba imekuwa hali ya kawaida katika karne ya 19 na 20 pale ambako utaratibu wa kifalme umeendelea. Mfalme hatekelezi tena shughuli za serikali. Serikali inachaguliwa na bunge kwenye msingi wa kura wa raia wote jinsi ilivyopangwa katika katiba ya nchi. Nafasi ya mfalme unafanana na ile ya rais katika jamhuri. Kuna tofauti kama mfalme ana athira katika siasa au kama cheo chake ni cha heshima tu na hana uwezo wa kuingilia kati katika kazi za bunge na serikali. Mifano yake ni wafalme wa Skandinavia au pia utaratibu wa Uingereza na nchi za Jumuiya ya Madola zisizo jamhuri. Nafasi ya mfalme iko hasa kama vikundi ndani ya bunga havikubaliani kuhusu serikali mpya na hakuna upande mwenye kura nyingi kabisa.

Wafalme wa nchi kama Moroko na Yordani wana athira kubwa zaidi.

• Mfalme mwenye mamlaka yote bila kufungwa na katiba alikuwa jambo la kawaida zamani lakini leo hii wamebaki wachache sana. Falme za aina ni Saudia, Omani, Qatar, Uswazi, Brunei na Bhutan (inayoandaa katiba kwa mwaka 2008).
• Mfalme wa sehemu ya taifa tu: mifano yake ni Kabaka wa Buganda au Asantehene wa Ashanti katika Ghana. Wafalme hawa wa jadi bado wanaheshimiwa na kuwa na athira kwa sababu wanatambuliwa na watu wao hata ndani ya jamhuri kubwa zaidi kuliko eneo la kabila au kundi lao.

Wafalme na watawala wengine

Hakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia mashariti kuhusu ukubwa wa eneo lake.

Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambako si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine kama watemi, machifu n.k.. Mara nyingi watawala wa Waswahili ambao hawakuwa na mamalaka nje ya eneo dogo la mji wao walijiita Sultani na Wareno waliwaita "reyes" (wafalme). Hali hii ililingana na mifano mingine kama kati ya Wagiriki wa Kale ambako vilevile watawala wadogo juu ya miji walitumia cheo cha "mfalme".

Tazama pia: Kaisari, Mtemi