Amanjena : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 1: Mstari 1:
'''Amanjena''' maana yake ni '''paradiso yenye amani'''. Ni hoteli ya kifahari na ya kupumzikia, inayopatikana Palmeraie kitongoji cha kusini mashariki mwa Marrakesh, [[Moroko]]. Ilijengwa mnamo mwaka 2000 na ni moja ya hoteli za kipekee na ya kwanza katika bara la Afrika. Ina mkondo wenye mashimo 21, maktaba iliyojaa vizuri na sehemu ya kuogelea ya nje, katikati ya vichaka vya hibiscus. Mnamo mwezi [[Mei]] mwaka [[2015]], [[David Beckham]] alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 40 katika hoteli hii.
'''Amanjena''' maana yake ni '''paradiso yenye amani'''. Ni hoteli ya kifahari na ya kupumzikia, inayopatikana Palmeraie kitongoji cha kusini mashariki mwa Marrakesh, [[Moroko]]. Ilijengwa mnamo mwaka [[2000]] na ni moja ya hoteli za kipekee na ya kwanza katika bara la Afrika. Ina mkondo wenye mashimo 21, maktaba iliyojaa vizuri na sehemu ya kuogelea ya nje, katikati ya vichaka vya hibiscus. Mnamo mwezi [[Mei]] mwaka [[2015]], [[David Beckham]] alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 40 katika hoteli hii.


== Usuli ==
== Usuli ==

Pitio la 20:13, 20 Juni 2021

Amanjena maana yake ni paradiso yenye amani. Ni hoteli ya kifahari na ya kupumzikia, inayopatikana Palmeraie kitongoji cha kusini mashariki mwa Marrakesh, Moroko. Ilijengwa mnamo mwaka 2000 na ni moja ya hoteli za kipekee na ya kwanza katika bara la Afrika. Ina mkondo wenye mashimo 21, maktaba iliyojaa vizuri na sehemu ya kuogelea ya nje, katikati ya vichaka vya hibiscus. Mnamo mwezi Mei mwaka 2015, David Beckham alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 40 katika hoteli hii.

Usuli

Amanjena ipo Palmeraie huko Marrakesh, kando ya barabara ya kwenda Ouarzazate, nje kidogo ya jiji la Marrakech linalolindwa na UNESCO katika eneo ambalo lipo katika mabonde ya mito ya Draa na Dadès imeungana na jangwa la Sahara.[1] Hoteli hii imejengwa nyuma ya kilima ambacho kinainuka kwa urefu wa futi 13000, katika mazingira ya shamba la mizeituni la Almoravid. Kuna muonekano wa Milima ya Atlas.[2]

Sinema ya mwaka 2010 ijulikanayo kama Sex and the City 2 ilichukuliwa huko Amanjena. Mnamo mwezi Mei mwaka 2015, David Beckham alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 40 katika hoteli hii,[3] pamoja na wageni Gordon Ramsay na Tana Ramsay, David Gardner na Liv Tyler, Spice Girls, Eva Longoria, Tom Cruise, David Blaine, Guy Ritchie na Vanessa Feltz.[4]

Ujenzi

Amanjena ilibuniwa na msanifu wa majengo Ed Tuttle, na kujengwa kwa kipindi cha miaka miwili. Ujenzi wa Moorish [3] upo katika mtindo wa jadi ya Kiarabu, yenye mabanda 32 na nyumba saba, na muundo wake wa ndani ni ya kisasa.[2] Ubunifu huo unajumuisha mitindo ya ujenzi wa Moorish katika mipangilio ya rangi yanayolingana na majengo ya Red City ya Marrakesh. Muundo huo ni wa jiwe, rangi ya tunda la tipisi, na rangi ya waridi, asali na rangi ya kijani ya sage iliyotumika katika jengo lote.[2]

Mlango mkubwa wa kuingilia unamuundo wa kale wa Kiarabu. Amanjena ina ushawishi mkubwa sana kwa mtindo wa Moorish, na ina chemchemi zenye rangi za jade. Ushawishi huo unamuundo wa mistari ya caravanserai na Ogres, na mabango ambayo hufunguliwa kuwa sehemu za maji. Sehemu zingine ni pamoja na paa lenye mwonekano wa mchanganyiko wa udongo wa ufinyanzi na mchanga, kumbi mbili zilizohifadhiwa kwa ajili ya mapumziko, varanda za ndani zenye mwelekeo wa chemchemi, nguzo zilizo chongwa, vigae vya kung'ara vya Moroko, na mapambo ya muundo wa ziggurat. Mbinu mbalimbali za upambaji zilitumika, kama vile écaille de poisson kwa zellige na plâtre ciselé katika kuta.[2]

Vyumba vina dari kubwa na vimewekwa mazulia ya Berber na taa. Kumbi nane zina bustani binafsi na mabwawa ya kuogelea. Nyumba zilijengwa kwa muundo wa nyumba za miji ya Moroko. Amanjena ina maktaba,[2] na migahawa miwili. Mgahawa kuu inadari yenye urefu wa mita sita na nguzo 80 zilizotengenezwa kwa onyx, wakati mgahawa mwingine unauza vyakula vya Kijapani. Mbali na bwawa la kuogelea, kuna chumba cha mazoezi.

Marejeo

  1. "Amanjene, Luxe Travel". 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 "Amanjena hotel, Marrakesh, Morocco: review". 
  3. 3.0 3.1 "David Beckham's 40th birthday party hotel - in pictures", 3 May 2015. 
  4. "David Beckham's birthday: Liv Tyler, Gordon Ramsay and Vanessa Feltz touch down in Marrakesh ahead of party". The Mirror. 3 May 2015. Iliwekwa mnamo 3 May 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)