Joseph Kabila : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: bg:Жозеф Кабила
Mstari 26: Mstari 26:
[[Category:Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]]
[[Category:Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo]]


[[bg:Жозеф Кабила]]
[[br:Joseph Kabila]]
[[br:Joseph Kabila]]
[[cs:Joseph Kabila]]
[[cs:Joseph Kabila]]

Pitio la 21:14, 10 Machi 2008

Joseph Kabila

Joseph Kabila Kabange (* 4 Juni 1971) ni rais wa nne wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Aliingia katika uraisi baada ya kifo cha babake Rais Laurent-Desiree Kabila aliyeuawa na wanajeshi tar. 16 Januari 2001. Wanasiasa wengine walimteua mwana kuwa raisi badala ya baba.

Katika uchaguzi wa kitaifa wa 30 Julai 2006 alipata kura nyingi kuwa raisi lakini hakufikia nusu ya kura zote. Katika uchaguzi wa pili kati yeye na Jean-Pierre Bemba alishinda akathebitishwa kuwa rais tar. 17 Novemba 2006. Joseph Kabila ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyechaguliwa na wananchi wote katika uchaguzi huru.

Maisha yake

Joseph Kabila alizaliwa mjini Hewa Bora mkoani wa Kivu Kusini katika mashariki ya Kongo. Babake alikuwa mwanasiasa na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo waasi waliopinga serikali ya Mobutu Sese Seko.

Pamoja na familia ya baba Joseph alihamia Dar es Salaam (Tanzania. Alisoma shule ya msingi na ya sekondari katika Daressalaam na Mbeya. Anasemekana alitumia wakati ule jina la Hippolyte Kanambe Kazemberembe Kabange Mtwale kwa sababu za usalama.

1996 alijiunga na wanamigambo ya babake katika vita ya Kongo ya Mashariki.

Baada ya ushindi wa wapinzani dhidi ya Mobutu baba alikuwa rais na Joseph alipelekwa masomoni kwenye chuo cha kijeshi huko Uchina. Wakati wa kurudi alipewa cheo cha jenerali jeshini na mwaka 2000 alipandishwa cheo kuwa mkuu wa jeshi.

Tangu kuwa raisi mwaka 2001 Joseph Kabila alijitahidi kumaliza hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe Kongo akakubali kufika kwa walinzi wa amani wa UM.

Desemba 2002 alikubali mapatano ya amani kati ya serikali na waasi yaliyokuwa msingi kwa ajili ya kuundwa kwa serikaliy a umoja wa kitaifa na maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2006.

Katika Juni 2006 alimwoa Olive Lembe di Sita aliyekuwa mchumba wake wa miaka mingi na mama wa binti aliyezaliwa 2001.