Peloponesi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Tag: 2017 source edit
Mstari 10: Mstari 10:
== Jiografia ==
== Jiografia ==
[[Picha:Corinth, Greece (NASA).jpg|thumb|300px|Shingo la nchi ya Korintho, mji wa Korintho upande wa kushoto, mstari nyoofu wa Mfereji wa Korintho katikati ya picha]]
[[Picha:Corinth, Greece (NASA).jpg|thumb|300px|Shingo la nchi ya Korintho, mji wa Korintho upande wa kushoto, mstari nyoofu wa Mfereji wa Korintho katikati ya picha]]
Ghuba ya Korintho inatenganisha Peoponesi na Ugiriki bara.
Ghuba ya Korintho inatenganisha Peloponesi na Ugiriki bara.


Rasi hiyo ina milima mingi na pwani lenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 [[juu ya UB]]. Rasi yote inakabiliwa na [[mitetemeko ya ardhi]] ya mara kwa mara.
Rasi hiyo ina milima mingi na pwani lenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 [[juu ya UB]]. Rasi yote inakabiliwa na [[mitetemeko ya ardhi]] ya mara kwa mara.

Pitio la 10:20, 10 Machi 2021

Peloponesi katika Ugiriki

Peloponesi (Kigiriki Πελοπόννησος peloponesos ) ni rasi kwenye kusini ya Ugiriki . Imeunganishwa na sehemu ya bara ya nchi kwa shingo la nchi pale kwenye mji wa Korintho.

Jina la kihistoria ya rasi lilikuwa Morea (Μωριάς morias).

Eneo lote la Peloponesi ni kilomita za mraba 21,549. Kuna watu 1,155,000 walioishi hapa kwenye mwaka 2011.

Peninsula imegawanywa kati ya mikoa mitatu ya kiutawala: sehemu kubwa ni ya mkoa wa Peloponnese, na sehemu ndogo ni za mkoa wa Ugiriki Magharibi na Attica .

Jiografia

Shingo la nchi ya Korintho, mji wa Korintho upande wa kushoto, mstari nyoofu wa Mfereji wa Korintho katikati ya picha

Ghuba ya Korintho inatenganisha Peloponesi na Ugiriki bara.

Rasi hiyo ina milima mingi na pwani lenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 juu ya UB. Rasi yote inakabiliwa na mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.

Mji mkubwa zaidi ni Patras yenye wakazi 170,000.

Miji

Miji mikubwa zaidi ya kisasa kwenye Peloponesi ni (sensa ya 2011):

  • Patras - wenyeji 170,896
  • Kalamata - wenyeji 62,409
  • Korintho - wenyeji 38,132
  • Tripoli - wenyeji 30,912
  • Aigio - wenyeji 26,523
  • Pyrgos - wenyeji 25,180
  • Argos - wenyeji 24,700
  • Sparta - wenyeji 19,854
  • Nafplio - wenyeji 18,910

Historia

Lango la Simba huko Mikeke (Mycenae) .
Hekalu la Hera, Olimpia .

Rasi hii iliona vipindi na watendaji muhimu katika historia ya Ugiriki ya Kale.

  • Ustaarabu wa Mikene ulistawi manmo mwaka 1600 KK - 1100 KK ulikuwa eneo la maendeleo ya tekinolojia ya zama za bronzi katika Ulaya. Mikene ilikuwa mji kwenye kaskazini ya Peloponesi.
  • Tangu mwaka 776 KK Michezo ya Olimpiki ilifanyika Olimpia kwenye magharibi mwa Peloponesi.
  • Miji mikubwa ya kale Sparta, Korintho, Argos na Megalopolis zote zilikuwa kwenye Peloponesi na kwa muda mrefu ilishirikiana katika Shirikisho la Peloponesi.
  • Kwenye miaka 431 KK - 404 KK vita ya Peloponesi iliona mapogano makali kati ya Sparta na Atheini.
  • Tangu mwaka 146 KK Peloponesi pamoja na Ugiriki yote ilikuja chini ya utawala wa Dola la Roma. Pamoja na sehemu zingine za Roma ya Kale hata hapa watu wengi walipokea dini mpya ya Ukristo.
  • Baadaya kuporomoka kwa Dola la Rome makabila ya Waslavi walianza kuhamia Peloponesi; baada ya karne kadhaa Waslavi hao walikuwa wameshapokea Ukristo na kutumia lugha ya Kigiriki[1]

Katika karne ya 15 Milki ya Osmani ilianza kuvamia Ugiriki na hadi mwaka 1532 hivi Ugiriki wote pamoja na Peloponesi ilikuwa chini ya Milki ya Osmani.[2]

  • Mwaka 1821 Vita ya Uhuru wa Ugiriki ilianza Kalamata kwenye Peloponesi [3] ikaendelea hadi kutambuiwa kwa Ugiriki kuwa nchi huru mnamo 1830..

Marejeo

  1. Stamatoyannopoulos, George et al., Genetics of the Peloponnesian populations and the theory of extinction of the medieval Peloponnesian Greeks, European Journal of Human Genetics, 25.5 (2017), pp. 637–645
  2. Bées & Savvides (1993), p. 239
  3. Richard Clogg (20 June 2002). A Concise History of Greece. Cambridge University Press. pp. 35–42. ISBN 978-0-521-00479-4. 

 

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Peloponesi travel guide kutoka Wikisafiri

Jamii:Ugiriki