Viti maalum vya wanawake : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8
Rescuing 2 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.8
Mstari 25: Mstari 25:


==Marejeo==
==Marejeo==
*[http://www.quotaproject.org/aboutProject.cfm Tovuti ya quotaproject.org] (mradi wa International IDEA, Inter-Parliamentary Union na Chuo Kikuu cha Stockholm)
*[http://www.quotaproject.org/aboutProject.cfm Tovuti ya quotaproject.org] {{Wayback|url=http://www.quotaproject.org/aboutProject.cfm |date=20170314195207 }} (mradi wa International IDEA, Inter-Parliamentary Union na Chuo Kikuu cha Stockholm)
*[http://www.quotaproject.org/atlas.pdf Atlas of Electoral Gender Quotas]
*[http://www.quotaproject.org/atlas.pdf Atlas of Electoral Gender Quotas] {{Wayback|url=http://www.quotaproject.org/atlas.pdf |date=20170423123517 }}





Pitio la 04:46, 15 Februari 2021

Viti maalum vya wanawake ni utaratibu unaopatikana katika nchi mbalimbali unaolenga kuongeza idadi ya wanawake na athira yao katika bunge na mabaraza kwahiyo katika siasa kwa jumla ya nchi hizi.

Kuna nchi nyingi za dunia zilizochukua hatua za kuongeza nafasi za wanawake serikalini kulingana na Mkataba kuhusu ufutaji wa ubaguzi wote wa wanawake (Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women) uliosainiwa na mataifa 189 tangu kuanzishwa mwaka 1981 na kuimarishwa na azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2011. [1].

Nchi zinazotumia utaratibu wa viti maalumu vya wanawake katika bunge zao

Kati ya hatua hizi ni utaratibu wa kisheria wa kutenga sehemu ya viti vya bunge za kitaifa kua kwa wanawake pekee. Mnamo mwaka 2013 utaratibu huu ulitumiwa katika nchi 36, hasa za Afrika na Asia Kusini.

Katika Amerika ni nchi ya Haiti.

Katika Afrika ni nchi za Algeria, Burundi, Djibouti, Eritrea, Guinea, Kenya, Lesotho, Libya, Mauritania, Morocco, Niger, Rwanda, Sierra Leone, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Uswazi na Zimbabwe.


Katika Asia ni nchi za Afghanistan, Bangladesh, China, India, Iraq, Jordan,Palestina, Saudi Arabia, Pakistan, Philippines, Samoa, Taiwan, Timor-Leste na Vanuatu.

Mifumo mbalimbali

Nchi nyingi hutenga idadi ya viti vya wabunge kwa ajili ya wanawake wanaochaguliwa kwa namna za pekee. Mara nyingi wananchi hupiga kura mara mbili, kwanza kwa wawakilishi wao kwa jumla halafu kura ya pili kwa ajili ya wanawake pekee.

Kuna pia nchi ambazo zimeanzisha majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya wagombea wanawake pekee.

Nchi chache hutumia mfumo kama Tanzania ambako takriban theluthi 1 ya viti kwenye bunge ni viti maalumu ya wanawake wanaoingia baada ya kutajwa na vyama vya kisiasa lakini bila kupigiwa kura.[2]

Tanbihi

  1. Resolution adopted by the General Assembly on 19 December 2011 - 66/130 Women and political participation, Tovuti ya Umoja wa Mataifa undocs.org, iliangaliwa Mei 2017
  2. "Fungu 66, 1b ya Katiba ya Tanzania". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-05-16. Iliwekwa mnamo 2017-05-15. 

Marejeo