Polandi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
No edit summary
Mstari 146: Mstari 146:
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Umoja wa Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Umoja wa Ulaya]]
[[Jamii:Mkataba wa Schengen]]

Pitio la 17:10, 13 Desemba 2020

Polandi

Poland (kwa Kipoland: Polska) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani upande wa magharibi, Ucheki na Slovakia upande wa kusini, Ukraine na Belarus upande wa mashariki na Bahari ya Baltiki, Lituanya na Urusi (mkoa wa Kaliningrad Oblast) upande wa kaskazini.

Jiografia

Ardhi ya Poland ni tupu tu kufikia kiasi cha Bahari ya Baltiki katika upande wa kaskazini mwa Milima ya Carpathi kusini mwa nchi. Ndani ya eneo hilo lililo tupu, ardhi inatofautiana kutoka mashariki na magharibi.

Pwani ya Kipolandi ya Bahari ya Baltiki ni murua zaidi, lakini ina bandari asilia katika mkoa wa Gdańsk-Gdynia na Szczecin huko mashariki-magharibi ya mbali. Pwani hiyo ina upepo mzuri na maeneo kadhaa ya pwani za maziwa. Pwani za maziwa na fukwe za zamani ambazo zimekatwa kutoka baharini. Sehemu hizi pia huitwa rasi. Rasi ya Szczecin ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa nchi ya Ujerumani. Rasi ya Vistula ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa mji wa Kaliningrad, ambao ni katika mkoa wa Urusi.

Mto mrefu zaidi nchini Poland ni Vistula, unaoangukia ndani ya Rasi ya Vistula na pia unakwenda moja kwa moja hadi katika Bahari ya Baltiki. Ni km 1064 kutoka chanzo hadi mdomo.

Kanda ya kaskazini-mashariki ni miti tu imejaa, inakosa watu wachache na rasilimali za kilimo na viwanda. Kanda ya kijografia ina wilaya nne za vilima vya moraine na maziwa yaliyotengenezwa na moraine. Haya yalianzishwa baada ya Pleistocene Zama za Barafu. Ziwa Masurian ni miongoni mwa maziwa manne ya wilaya yaliyochukua eneo kubwa la kaskazini-mashariki mwa Poland.

Poland ina maziwa kibao. Kwa Ulaya nzima, Finland peke yake ina maziwa mengi zaidi. Maziwa makubwa ni "Śniardwy" na "Mamry". Kwa kuongeza katika wilaya ya ziwa katika kaskazini, kuna idadi kubwa pia ya mlima maziwa katika milima ya Tatra.

Kusini mwa kanda ya kaskazini-mashariki mwa mikoa ya Silesia na Masovia, ambapo kuna alama za mto na mabonde ya zama za barafu. Mkoa wa Silesia una rasilimali nyingi na watu wengi. Kuna makaa ya mawe tele. Silesia ya Chini ina mgodi wa shaba mkubwa kabisa. Tambarare ya Masovian ipo kati ya Poland. Ipo katika mabonde ya mito mikubwa mitatu: Vistula, Bug na Narew.

Ukiendelea na safari kusini ni mlima ya kanda ya Kipolandi. Milima hiyo ni pamoja na Sudetes na Milima ya Carpathi. Sehemu ndefu ya Carpathia ni milima ya Tatra ambayo imekwenda hadi kusini mwa mpaka wa nchi ya Poland.

Mlima mrefu zaidi nchini Poland unaitwa "Rysy" wenye m 2,503 (ft 8,210), upo Tatras.

Historia

Ramani ya Polandi chini ya Mieszko I, mwanzilishi wa taifa (960–992).
Shirikisho la Warsaw katika kilele cha uenezi wake (1635).

Waslavi walienea kati nchi katika nusu ya pili ya karne ya 5 BK.

Ukristo wa Kikatoliki kupokewa na mfalme Mieszko I (960-992) na Wapolandi kwa jumla (966) hutazamiwa kama chanzo cha taifa lao la pekee katika jamii ya Waslavi.

Nchi ilistawi na kuenea hasa chini ya ukoo wa Jageloni (13861572).

Kuanzia mwaka 1764 nchi ilianza kurudi nyuma na zile za jirani ziligawana kwa awamu tatu (1772, 1793, 1795) eneo lake lote.

Wapolandi walijaribu mara kadha kujikomboa, lakini walipata uhuru kwa muda tu (1807-1815 na 1918-1939).

Baada ya vita vikuu vya pili, Polandi ikawa chini ya utawala wa Kikomunisti hadi ilipofaulu kujikomboa (1989).

Poland imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

Watu

Wakazi ni 38,483,957, karibu wote wakiwa Wapolandi asili (93.52%), wakiongea Kipolandi na wakifuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (87.5%), tena kwa bidii ya pekee.

Kati ya lugha nyingine zilizotambulika kisheria, zinaongoza Kikashubi na Kijerumani, halafu Kibelarusi na, Kiukraina. Kati ya lugha za kigeni zinaongoza Kiingereza na Kirusi.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Kurasa za taasisi za serikali

Utalii Poland

Kurasa mtandaoni juu ya Poland

Habari za Poland kwa Kiingereza


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Poland bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Polandi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.