Dubai : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
+image #WPWP #WPWPTZ
Tag: Reverted
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Dubaicollage.jpg|thumbnail|right|200px|Muonekano wa Mji wa Dubai]]

'''Dubai''' (kwa [[Kiarabu]]: دبيّ) ni [[ufalme]] katika [[Shirikisho]] la [[Falme za Kiarabu]] kwenye [[rasi ya Uarabuni]] na pia [[jina]] la [[mji mkuu]] wa ufalme huo.
'''Dubai''' (kwa [[Kiarabu]]: دبيّ) ni [[ufalme]] katika [[Shirikisho]] la [[Falme za Kiarabu]] kwenye [[rasi ya Uarabuni]] na pia [[jina]] la [[mji mkuu]] wa ufalme huo.



Pitio la 06:11, 19 Julai 2020

Faili:Dubaicollage.jpg
Muonekano wa Mji wa Dubai

Dubai (kwa Kiarabu: دبيّ) ni ufalme katika Shirikisho la Falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni na pia jina la mji mkuu wa ufalme huo.

Amiri wa Dubai, ambaye ni pia Makamu wa Rais wa shirikisho, ni Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Dubai ni ufalme mkubwa wa pili katika shirikisho hilo baada ya Abu Dhabi.

Iko kwenye mwambao wa Ghuba ya Uajemi kati ya Sharjah na Abu Dhabi.

Mji wa pili ni Hatta mpakani kwa Oman.

Jiji la Dubai lilikuwa mji mdogo wenye wakazi 20,000 tu hadi vita kuu ya pili ya dunia. Leo hii kuna wakazi zaidi ya 1,200,000. Nyumba zote za Dubai ni mpya.

Kukua kwa Dubai kulianzishwa kutokana na mapato ya mafuta ya petroli. Lakini akiba za mafuta hayo si kubwa kama kwa majirani yake. Mapato ya mafuta ni 6% pekee za pato la taifa.

Viongozi wa Dubai wamefaulu kuweka msingi mpya wa uchumi katika biashara na utalii.

Tazama pia

Viungo vya nje