Machakos : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Machakos Country Bus
Mstari 31: Mstari 31:
Mwaka [[2002]] [[majadiliano]] kati ya pande mbalimbali za [[vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan]] yalifanyika Machakos.
Mwaka [[2002]] [[majadiliano]] kati ya pande mbalimbali za [[vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan]] yalifanyika Machakos.


Kituo kikuu cha [[mabasi]] mjini Nairobi huitwa na wenyeji "''Machakos Airport''".
Kituo kikuu cha [[mabasi]] mjini Nairobi huitwa na wenyeji "''Machakos Country Bus''".


==Tanbihi==
==Tanbihi==

Pitio la 10:10, 3 Juni 2020


Machakos
Machakos is located in Kenya
Machakos
Machakos

Mahali pa mji wa Machakos katika Kenya

Majiranukta: 1°31′0″S 37°16′0″E / 1.51667°S 37.26667°E / -1.51667; 37.26667
Nchi Kenya
Kaunti za Kenya Machakos
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 150,041

Machakos ni mji wa Kenya (Ukambani) takriban kilomita 64 upande wa kusini-mashariki wa Nairobi. Ni makao makuu ya kaunti ya Machakos.

Machakos imekua haraka kwa sababu ni karibu na mji mkuu wa taifa imeshapita idadi ya wakazi lakhi moja na nusu[1]. Wenyeji wa Machakos ni hasa Wakamba.

Historia

Machakos ni kati ya miji ya kwanza ya Kenya bara ikaundwa mwaka 1899 na Waingereza na kuwa makao makuu ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (mbali na eneo lindwa la pwani lililokodishwa na Usultani wa Zanzibar na Uingereza) kwa muda mfupi.

Jina la mji lilitokana na chifu Masaku wa Wakamba aliyewahi kuwa na boma lake hapo.

Baada ya azimio la kutounganisha Machakos na reli ya Uganda mji haukuendelea sana.

Mwaka 2002 majadiliano kati ya pande mbalimbali za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan yalifanyika Machakos.

Kituo kikuu cha mabasi mjini Nairobi huitwa na wenyeji "Machakos Country Bus".

Tanbihi

  1. Sensa ya Kenya 2009, tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.

Viungo vya nje