Jokate Mwegelo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3: Mstari 3:
|majina mengine = Jojo Kidoti
|majina mengine = Jojo Kidoti
|picha= Jokate mwegelo.jpg
|picha= Jokate mwegelo.jpg
|caption =
|caption = Jokate akiwa katika picha ya kiofisi
|mahali pa kuzaliwa = Washington, D.C. <small>[[Marekani]]</small>
|mahali pa kuzaliwa = Washington, D.C. <small>[[Marekani]]</small>
|tarehe ya kuzaliwa = 20 Machi 1987
|tarehe ya kuzaliwa = 20 Machi 1987

Pitio la 07:40, 2 Aprili 2020

Jokate Mwegelo
Amezaliwa20 Machi 1987
UtaifaMtanzania
Majina mengineJojo Kidoti
MhitimuChuo Kikuu cha Dar Es Salaam (Shahada ya Sayansi ya Siasa)
Kazi yakemwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji, mwanasiasa
Miaka ya kazi2006-hadi sasa

Jokate Mwegelo (amezaliwa 20 Machi 1987) ni mwigizaji wa filamu, mjasiriamali na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania. Mwezi Julai 2018 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Jokate vilevile alikuwa mtangazaji na mwimbaji[1][2][3][4] pia alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.[5][6]

Mwaka 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji filamu bora wa kike.[7].Mwaka 2017, Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.[8]

Maisha ya awali na elimu

Jokate Mwegelo alizaliwa jijini Washington, D.C, Marekani, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.

Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio Primary School na baadaye St. Anthony High School, halafu Loyola High School, Dar es Salaam.

Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.

Miss Tanzania 2006

Alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.[9] Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds fashion na balozi wa gazeti la Citizen, baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.[4]

Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006, shindano ambalo alishinda, kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006, ambako pia alishinda.[10]

Kazi

Mwaka 2018 ateuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa mkuu wa wilaya ya kisarawe

Kuigiza

Mwaka wa 2007, alipata kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors, akiwa na Vincent Kigosi, Lisa Jensen, mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na marehemu Adam Kuambiana.[11]

Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With True Love[12]

Mwaka wa 2010, alionekana katika filamu ya Chumo, filamu iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria.[13] Filamu hii ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards.

Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa TV maarufu wa Siri Ya Mtungi, uliokuwa unaandaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani, mnamo 2013.[14] Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa "Ndekwa" katika filamu ya Mikono Salama, ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.[15]

Kampuni ya Kidoti

Muziki

Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa na A.Y. katika wimbo wa Kings and Queen, na Amani, kutoka Kenya. Mwaka wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci, uliyoitwa 'Kaka na Dada.[16][17] Mwaka wa 2015, akadondosha wimbo wake mwingine uliyoitwa Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.[18]

Siasa

Jokate hakujulikana kujishughulisha na siasa hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) kuongoza Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya umoja huu akiwa kaimu katibu wa idara hii. Yeye mwenyewe alitaja maarifa ya utoto wake alipohamasishwa na bibi yake aliyekuwa mwasisi wa Umoja wa Walimu Tanzania katika Mkoa wa Rukwa kuona ni muhimu kujitoa katika jamii na kuchukua nafasi za uongozi. [19] Wakati ule magazeti yalileta taarifa kuwa uteuzi wake ulipingwa na sehemu ya viongozi wa umoja huu.[20]

Kwenye mwezi wa Machi 2018 aliondolewa katika nafasi hii kwa azimio la kamati kuu ya UVCCM.[21]

Mwisho wa mwezi wa Julai 2018 aliteuliwa na rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe[22], uteuzi ambao ulileta cheche nyingi katika uwanja wa mitandao nchini Tanzania. Wapo waliobeza uteuzi huo, wapo waliosifia. Wengine waliweka picha zake za zamani zilizokuwa hazina maadili ili kukebehi uteuzi huo.[23]

Filamu

  • Movies
Mwaka Filamu Uhusika Washiriki
2007 Fake Pastors[24] Jackie Vincent Kigosi, Adam Kuambiana, Lisa Jensen na Ahmed Ulotu
2008 From China With Love [25] Vincent Kigosi, Blandina Chagula, Suzan Lewis na Aileen Francisco
2011 Chumo[26] Amina Yusuph Mlela, Hussein Mkiety (Sharobaro)
2014 Mikono Salama[27] Ndekwa Jacob Steven, Single Mtambalike na Irene Uwoya
  • Mfululizo wa TV
Mwaka Mfululizo Uhusika Maelezo
2013-2014 Siri Ya Mtungi Msimu wa 2[28] Mwanamitindo

Diskografia

  • 2013

Kaka Dada akiwa na Lucci

  • 2015

Leo Leo akiwa Ice Prince

Marejeo

  1. YManager (20 August 2016). 'I keep pushing myself so I will leave a mark...' - Leading Ladies Africa speaks to Jokate Mwegelo of Kidoti - YNaija. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  2. Joketi Mwegelo - Actor, Model, Singer, — Bongo Movies. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  3. Channel O VJ: Jokate - Channel O TV Online (17 October 2011). Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  4. 4.0 4.1 Happy Birthday Jokate Mwegelo ( watch video + her Biography inside) - Bongo5.com. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  5. BongoToday.com - Entertainment and Lifestyle : Kidoti partners with Rainbow Shell Craft Company from China. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  6. VJ Blog: KidOti - Define Your Beauty - Channel O TV Online (24 May 2012). Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  7. http://www.africultures.com/php/index.php?nav=murmure&no=7524
  8. https://www.forbesafrica.com/people30/jokate-mwegelo/
  9. Blog, Michuzi (6 August 2006). MICHUZI BLOG: miss tz 2006. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  10. Blog, Michuzi (25 June 2006). MICHUZI BLOG: miss temeke 2006. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  11. Fake Pastors — Bongo Movie - Tanzania. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  12. From China With Love — Bongo Movie - Tanzania. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  13. Chumo Home. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  14. Saleem, Trim (25 November 2013). SWP: BEHIND THE SCENES: JOKATE, MONALISA AND RICHA ADHIA IN SIRI YA MTUNGI SEASON 2.. Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  15. ZIFF 2015: The winners (26 July 2015). Iliwekwa mnamo 6 September 2016.
  16. http://www.bongo5.com/picha-jokate-na-lucci-ni-kaka-na-dada-tu-08-2013/
  17. http://www.bongo5.com/photos-jokate-and-lucci-to-release-their-long-awaited-surprise-tonight-08-2013/
  18. http://vmgafrica.com/jokate-ft-ice-prince-leo-leo-audio/
  19. JOKATE: UVCCM LAZIMA IBADILIKE KUANGALIA CHANGAMOTO ZA VIJANA. mtanzania.co.tz ya tarehe Jun 28th, 2017. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
  20. JOKATE AIVURUGA UVCCM (sw). mtanzania.co.tz ya tarehe 24 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
  21. SABABU ZA KUTUMBULIWA JOKATE ZATAJWA (en-US). mtanzania.co.tz ya tarehe 25 MAchi 2018. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
  22. "Jokate, Kafulila, Katambi among loyalists Magufuli rewards in", The Citizen ya tarehe 30 Julai 2018 (in English), 2018-07-29, retrieved 2018-07-30 
  23. https://lemutuz.com/2018/07/31/usiyoyajua-kuhusu-jokate-dc-mpya-kisarawe/
  24. http://www.bongocinema.com/movies/view/fake-pastors
  25. http://www.bongocinema.com/movies/view/from-china-with-love
  26. http://www.bongocinema.com/movies/view/chumo
  27. http://www.bongo5.com/video-trailer-ya-mikono-salama-aliyocheza-jokate-jb-uwoya-na-richie-01-2014/
  28. http://www.bongo5.com/jokate-kuigiza-kwenye-msimu-wa-pili-wa-tamthilia-ya-siri-ya-mtungi-11-2013/

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jokate Mwegelo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.