Seaborgi : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
d Protected "Seaborgi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho)) |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 12:22, 16 Machi 2020
Seaborgi (seaborgium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Seaborgi (seaborgium) |
Alama | Sg |
Namba atomia | 106 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 269 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 12, 2 |
Densiti | 35 g/cm³ (kadirio) |
Ugumu (Mohs) | -- |
Asilimia za ganda la dunia | 0 % (elementi sintetiki) |
Hali maada | inaaminiwa ni mango |
Mengineyo | tamburania, nururifu |
Seaborgi (ing. seaborgium) ni elementi sintetiki iliyo na alama Sg na namba atomia 106. Imepokea jina lake kwa heshima ya mwanakemia wa Marekani Glenn T. Seaborg . Ilhali ni elementi sintetiki, haitokei kiasili katika mazingira yetu lakini inaweza kuundwa katika maabara. Ni dutu nururifu; isotopi yake iliyo thabiti zaidi inaitwa 269 Sg, ikiwa na nusumaisha ya dakika 14 hivi.
Atomu za kwanza za seaborgi zilitengenezwa mwaka 1974 katika maabara huko Umoja wa Kisoyeti na Marekani. Pande zote mbili zilivutana kwa miaka kadhaa kuhusu kipaumbele wa ugunduzi na haki ya kuamulia jina, hadi mwaka 1997 Jumuiya ya Kimataifa ya Kemia (IUPAC) iliamua jina rasmi kuwa "seaborgium".
Tabia nyingi hazijulikani kwa sababu mbili
a) elementi hii inapatikana tu baada ya kutengenezwa katika maabara kwa gharama kubwa [1]
b) baada ya kupatika inaachana haraka haidumu
Marejeo
- ↑ Subramanian, S. "Making New Elements Doesn’t Pay. Just Ask This Berkeley Scientist". Bloomberg Businessweek. Iliwekwa mnamo 2020-01-18.
- ↑ Barber, Robert C.; Gäggeler, Heinz W.; Karol, Paul J.; Nakahara, Hiromichi; Vardaci, Emanuele; Vogt, Erich (2009). "Discovery of the element with atomic number 112 (IUPAC Technical Report)". Pure and Applied Chemistry 81 (7): 1331. doi:10.1351/PAC-REP-08-03-05.