Mcheduara : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16: Mstari 16:




[[Jamii:Jiometri]
[[Jamii:Jiometri]]

Pitio la 22:06, 11 Machi 2020

Kopo hili lina umbo la mcheduara
Mcheduara mraba na mshadhari
Mcheduara mraba

Mcheduara (ing. cylinder) ni gimba la kijiometri linalofanana na kopo au kipande cha pipa. Hivyo jina lake linaeleza ni mche mwenye umbo la duara au mviringo. Gimba la mcheduara linapakanwa na miduara bapa miwili inayokaa sambamba na kuwa vitako vyake.

Kihisabati mcheduara inaweza kufafanuliwa pia kama uso ambao ni jumla ya nukta zote zenye umbali sawa na mstari ilio katikati yake unaojulikana kama "mhimili" wake. Hii ni bila kitako.

Kutokana na ufafanuzi huo gimba la mchemraba ni umbo thabiti uliomo ndani ya uso huo ukipakanwa na vitako viwilibapa sambamba.

  • Kama vitako vinakaa kwa pembemraba juu ya mhimili, mcheduara huitwa mraba.
  • Kama vitako vinakaa kwa pembe tofauti, tunapata mcheduara mshadhari.

Mcheduara mraba huwa na

  • mjao V = π r 2 h
  • eneo la uso bila bapa zinazopakana M = 2 π r h
  • eneo la uso wote E = 2 π r 2 + 2 π r h