Virusi vya Corona : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit Advanced mobile edit
Mstari 11: Mstari 11:


==SARS==
==SARS==
SARS ''(Severe acute respiratory syndrome)'' ilikuwa ugonjwa sugu wa mfumo wa upumuo uliosababishwa na virusi vya corona aina ya SARS-CoV. Uliripotiwa mara ya kwanza huko [[Asia]] kwenye Februari [[2003]] ukaendelea kusambaa katika miezi iliyofuata katika nchi zaidi ya 20 katika [[Amerika]], [[Ulaya]] na Asia hadi kwisha. Ugonjwa ulianza kuonekana kwa [[homa]] juu ya [[C°]] 38, [[maumivu]] ya [[kichwa]] na kujisika dhaifu. [[Asilimia]] 10-20 za wagonjwa walihara. Wengi walioambukizwa waliendelea kupata [[nimonia]]. Kulikuwa na taarifa za watu 8,098 walioambukizwa, na 774 walifariki katika nchi 17<ref name="PMID 16978751">{{cite journal |doi=10.1016/j.socscimed.2006.08.004 |pmid=16978751 |title=Responding to global infectious disease outbreaks: Lessons from SARS on the role of risk perception, communication and management |journal=Social Science & Medicine |volume=63 |issue=12 |pages=3113–23 |year=2006 |last1=Smith |first1=Richard D }}</ref>, wengi wao nchini China. <ref name="who:table2004_04_21">{{cite web|url=http://www.who.int/csr/sars/country/table2004_04_21/en/index.html|title=Summary of probable SARS cases with onset of illness from 1 November 2002 to 31 July 2003|publisher=[[World Health Organization]] (WHO) |accessdate=31 October 2008}}</ref>
SARS ''(Severe acute respiratory syndrome)'' ulikuwa ugonjwa sugu wa mfumo wa upumuo uliosababishwa na virusi vya corona aina ya SARS-CoV. Uliripotiwa mara ya kwanza huko [[Asia]] kwenye Februari [[2003]] ukaendelea kusambaa katika miezi iliyofuata katika nchi zaidi ya 20 katika [[Amerika]], [[Ulaya]] na Asia hadi kwisha. Ugonjwa ulianza kuonekana kwa [[homa]] juu ya [[C°]] 38, [[maumivu]] ya [[kichwa]] na kujisika dhaifu. [[Asilimia]] 10-20 za wagonjwa walihara. Wengi walioambukizwa waliendelea kupata [[nimonia]]. Kulikuwa na taarifa za watu 8,098 walioambukizwa, na 774 walifariki katika nchi 17<ref name="PMID 16978751">{{cite journal |doi=10.1016/j.socscimed.2006.08.004 |pmid=16978751 |title=Responding to global infectious disease outbreaks: Lessons from SARS on the role of risk perception, communication and management |journal=Social Science & Medicine |volume=63 |issue=12 |pages=3113–23 |year=2006 |last1=Smith |first1=Richard D }}</ref>, wengi wao nchini China. <ref name="who:table2004_04_21">{{cite web|url=http://www.who.int/csr/sars/country/table2004_04_21/en/index.html|title=Summary of probable SARS cases with onset of illness from 1 November 2002 to 31 July 2003|publisher=[[World Health Organization]] (WHO) |accessdate=31 October 2008}}</ref>


SARS haijatokea tena tangu mwaka [[2004]].
SARS haijatokea tena tangu mwaka [[2004]].

Pitio la 19:15, 7 Februari 2020

Virusi vya Corona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ni kundi la virusi vinavyoweza kusababisha magonjwa kwa wanyama (mamalia na ndege) lakini pia kwa binadamu[1]. Inaaminiwa ni aina ya virusi vilivyohama kutoka kwa wanyama na kuathiri binadamu pia.

Virusi vya Corona vipo vya aina mbalimbali, zikiwemo 229E, NL63, OC43, na HKU1 [2].

Tabia za pamoja

Virusi vya corona huwa na uwezo wa kubadilika na aina nyingi husababisha magonjwa yasiyo hatari sana upande wa binadamu. Kudhoofika kwa mwili kutokana na mashambulio ya virusi kunafungua milango kwa bakteria wanaoleta maambukizo ya mfumo wa upumuo, kama mafua au homa ya mafua, yanayoishia kwa kawaida baada ya siku kadhaa, lakini kuna pia maambukizo ya hatari yanayoweza kusababisha kifo.

Hakuna chanjo au dawa ya kudhibiti virusi vya aina hii. Kwa hiyo uponyaji hutegemea mara kwa mara nguvu ya kinga mwilini cha kila mtu. Hii inamaanisha virusi hivi huleta hatari hasa kwa watu wenye kinga cha mwili kilichodhoofishwa.

Ilhali aina hizo za virusi zina uwezo wa kubadilika, miaka ya nyuma ilikuwa na mabadiliko kadhaa yaliyosababisha vifo vya watu na kuenea haraka kimataifa, hivyo kusababisha hofu za epidemiki au hata pandemia.

SARS

SARS (Severe acute respiratory syndrome) ulikuwa ugonjwa sugu wa mfumo wa upumuo uliosababishwa na virusi vya corona aina ya SARS-CoV. Uliripotiwa mara ya kwanza huko Asia kwenye Februari 2003 ukaendelea kusambaa katika miezi iliyofuata katika nchi zaidi ya 20 katika Amerika, Ulaya na Asia hadi kwisha. Ugonjwa ulianza kuonekana kwa homa juu ya 38, maumivu ya kichwa na kujisika dhaifu. Asilimia 10-20 za wagonjwa walihara. Wengi walioambukizwa waliendelea kupata nimonia. Kulikuwa na taarifa za watu 8,098 walioambukizwa, na 774 walifariki katika nchi 17[3], wengi wao nchini China. [4]

SARS haijatokea tena tangu mwaka 2004.

2019 Novel Coronavirus (2019-nCoV)

Mwisho wa mwaka 2019 uliona kutokea kwa badiliko jipya lililotambuliwa mara ya kwanza mjini Wuhan, China. [5]

Aina hiyo ya virusi vya corona iliitwa 2019 Novel Coronavirus (2019-nCoV). Usambazaji wake ulionekana kuanza kutokana na virusi vya wanyama vilivyofikia binadamu. Wagonjwa walionyesha matatizo kwenye njia ya upumuo; wengine waliathiriwa kidogo tu, lakini wengine waligonjeka vibaya hadi kufa. Dalili zilizotambuliwa hadi mwisho wa Januari 2020 ni pamoja na homa, kukohoa na ugumu wa kuvuta pumzi. Inaonekana dalili za ugonjwa zinaweza kuanza takriban siku 2 hadi 14 baada ya kuambukizwa. Walio hatarini zaidi ni watu waliodhoofishwa na magonjwa mengine au wenye mfumo dhaifu wa kinga mwilini kwa sababu nyingine, kwa mfano umri mkubwa.

Hadi mwisho wa Januari 2020 takriban watu 10,000 waliambukizwa, idadi ya vifo ilikuwa mnamo 200. Virusi vilienea hadi nchi nyingine kwa njia ya abiria wa ndege za kimataifa. Wakazi wa Wuhan na miji mingine ya China yenye wagonjwa wamekataliwa kuondoka kwao baada ya hali ya karantini kutangazwa.[6].

Ushauri wa kujikinga dhidi ya maambukizi

Maambukizi husambaa hasa kwa majimaji ya mwilini, kama matone madogo ya mate au chafya; mtu aliyeambukizwa atakuwa na virusi kwenye mikono yake akigusa pua au mdomo. Inawezakana mtu aliyeambukizwa haonyeshi dalili za ugonjwa bado lakini anaweza kupitisha virusi tayari.

Unashauriwa:

  • kunawa mikono mara kwa mara kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni. Ukiwa nayo tumia dawa yenye alikoholi (si chini ya asilimia 60) kusafisha mikono.
  • usiguse macho, pua na midomo kwa mikono kama hujanawa
  • epukana kuwa karibu sana na wagonjwa
  • kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga chako ni dhaifu katika hali hii)
  • tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya choo / toilet paper) uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
  • safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (pamoja na kikombe, deski, simu yako)[7]

Tanbihi

  1. Coronavirus (en). WebMD. Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
  2. Coronavirus | About | Symptoms and Diagnosis | CDC (en-us). www.cdc.gov (2020-01-25). Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
  3. Smith, Richard D (2006). "Responding to global infectious disease outbreaks: Lessons from SARS on the role of risk perception, communication and management". Social Science & Medicine 63 (12): 3113–23. PMID 16978751. doi:10.1016/j.socscimed.2006.08.004. 
  4. Summary of probable SARS cases with onset of illness from 1 November 2002 to 31 July 2003. World Health Organization (WHO). Iliwekwa mnamo 31 October 2008.
  5. Julia Naftulin, Business Insider. Wuhan Coronavirus Can Be Infectious Before People Show Symptoms, Official Claims (en-gb). ScienceAlert. Iliwekwa mnamo 2020-01-28.
  6. 5 million people left Wuhan before China quarantined the city to contain the coronavirus outbreak, taarifa ya gazeti Business Insider USA, kupitia www.pulselive.co.ke, tarehe 27-01-2020
  7. About prevention and treatment, tovuti ya National Center for Immunization and Respiratory Diseases (NCIRD), Division of Viral Diseases, Marekani, iliangaliwa 30 Januari 2020
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Virusi vya Corona kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.