Tabakamwamba : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Tafsir
Tags: Mobile edit Mobile web edit
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 1: Mstari 1:


[[Picha::Earth-cutaway-schematic-numbered.svg.png|thumb|350px| Muundo wa [[Dunia]]: 1: Ganda la Dunia (kibahari 1a na kibara 1b unene km 0 hadi 80); 2: Koti ya Dunia ; 3: Kiini cha Dunia; 3a: Kiini cha nje (kiowevu); 3b: Kiini cha ndani (thabiti); 4: Tabakamwamba (ganda pamoja na sehemu ya juu ya koti); 5: Asthenosphere]]
[[Picha::Earth-cutaway-schematic-numbered.svg|thumb|350px| Muundo wa [[Dunia]]: 1: Ganda la Dunia (kibahari 1a na kibara 1b unene km 0 hadi 80); 2: Koti ya Dunia ; 3: Kiini cha Dunia; 3a: Kiini cha nje (kiowevu); 3b: Kiini cha ndani (thabiti); 4: Tabakamwamba (ganda pamoja na sehemu ya juu ya koti); 5: Asthenosphere]]
[[Picha:Mabamba gandunia (tectonic plates).png|right|thumb|350px|Mabamba gandunia]]
[[Picha:Mabamba gandunia (tectonic plates).png|right|thumb|350px|Mabamba gandunia]]
'''Tabakamwamba''' (ing. ''lithosphere'')<ref>IPA: lith'usfēr,kutoka maneno ya [[Kigiriki]] λίθος ''líthos'' (jiwe, mwamba) na σφαίρα ''sfaira'' (tufe, tabaka)</ref> ni sehemu thabiti ya nje ya [[sayari]] ya Dunia. Hiyo inamaanisha [[ganda la Dunia]], pamoja na chini yake sehemu ya juu ya "koti ya dunia". Tabakamwamba inakaa juu ya sehemu moto na laini ya ndani zaidi ya koti ya Dunia.
'''Tabakamwamba''' (ing. ''lithosphere'')<ref>IPA: lith'usfēr,kutoka maneno ya [[Kigiriki]] λίθος ''líthos'' (jiwe, mwamba) na σφαίρα ''sfaira'' (tufe, tabaka)</ref> ni sehemu thabiti ya nje ya [[sayari]] ya Dunia. Hiyo inamaanisha [[ganda la Dunia]], pamoja na chini yake sehemu ya juu ya "koti ya dunia". Tabakamwamba inakaa juu ya sehemu moto na laini ya ndani zaidi ya koti ya Dunia.

Pitio la 05:29, 24 Desemba 2019

[[Picha::Earth-cutaway-schematic-numbered.svg|thumb|350px| Muundo wa Dunia: 1: Ganda la Dunia (kibahari 1a na kibara 1b unene km 0 hadi 80); 2: Koti ya Dunia ; 3: Kiini cha Dunia; 3a: Kiini cha nje (kiowevu); 3b: Kiini cha ndani (thabiti); 4: Tabakamwamba (ganda pamoja na sehemu ya juu ya koti); 5: Asthenosphere]]

Mabamba gandunia

Tabakamwamba (ing. lithosphere)[1] ni sehemu thabiti ya nje ya sayari ya Dunia. Hiyo inamaanisha ganda la Dunia, pamoja na chini yake sehemu ya juu ya "koti ya dunia". Tabakamwamba inakaa juu ya sehemu moto na laini ya ndani zaidi ya koti ya Dunia.

Kwenye mpaka kati ya tabakamwamba na koti yenyewe iko tabaka kasiduni (ing. asthenosphere) ambayo ni nyumbufu kiasi.

Tabakamwamba inafanywa na miamba imara, tofauti na sehemu za ndani zaidi ya Dunia ambako mwamba na madini yote vinapatikana kwa hali nyumbufu au giligili kutokana na joto kali na shinikizo kubwa.

Eneo la tabakamwamba linagawiwa kwa vipande vikubwa ambavyo vinaelea juu ya sehemu moto za ndani. Vipande hivi ni mabamba ya ganda la Dunia au kwa kifupi mabamba gandunia.

Aina za tabakamwamba

Kuna aina mbili za tabakamwamba:

  1. Tabakamwamba chini ya bahari; mabamba gandunia huachana katika vilindi vya bahari na hapa magma joto inapanda juu na kujenga hivyo miamba mipya ikipoa na kuganda. Hivyo ganda la Dunia chini ya bahari ina umri mdogo zaidi na unene mdogo wa kilomita 50-100.
  2. Tabakamwamba ya bara. Hapa tunakuta miamba ya kale zaidi na unene wake ni km 100 hadi 200.

Mzunguko wa tabakamwamba

Sehemu kubwa za tabakamwamba ziko katika mwendo wa kutokea na kupotea tena. Kenye vilindi vya bahari ambako mabamba gandunia yanaachana, magma inapanda na kuunda miamba mapya. Mchakato endelevu unasukuma mabamba jirani mbali kutoka mistari hii. Kwa upande mwingine kuna sehemu ambako mabamba yanasukumana na hapa bamba moja husukumwa chini ya bamba jingine na kwa namna hii kuunda mifereji ya bahari. Kadri miamba inazama chini na kuingia katika vilindi enye joto kubwa inayeyushwa tena na kujiunga na magma ya koti ya Dunia.


Marejeo

  1. IPA: lith'usfēr,kutoka maneno ya Kigiriki λίθος líthos (jiwe, mwamba) na σφαίρα sfaira (tufe, tabaka)

Vyanzo vingine

  • Ukoko wa ardhi, litholojia na anga
  • Ukoko na Lithosphere
  • Barrell J. 1914a, b & c. Nguvu ya ukoko wa Dunia. Jarida la Jiolojia. 22, 425-433; 441-468; 655-683.
  • Daly, R. 1940 Nguvu na muundo wa Dunia. New York: Jumba la Prentice.
  • Chernicoff, Stanley na Whitney, Donna. 2007. Jiolojia. utangulizi wa jiolojia ya mwili, 4th, Pearson 2007

Other websites