Bamba la gandunia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d wikidata interwiki
Mstari 11: Mstari 11:
Mabamba makubwa ya ganda la nje ya dunia ni:
Mabamba makubwa ya ganda la nje ya dunia ni:
*[[Bamba la Afrika]] - bara la [[Afrika]] pamoja na [[tako la bara]] baharini - ni [[bamba la kibara]]
*[[Bamba la Afrika]] - bara la [[Afrika]] pamoja na [[tako la bara]] baharini - ni [[bamba la kibara]]
*[[Bamba la Antaktika]] - bara la [[Antaktika]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara
*[[Bamba la Antaktiki]] - bara la [[Antaktiki]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara
*[[Bamba la Australia]] - bara la [[Australia]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara
*[[Bamba la Australia]] - bara la [[Australia]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara
*[[Bamba la Ulaya-Asia]] - mabara ya [[Ulaya]] na [[Asia]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara
*[[Bamba la Ulaya-Asia]] - mabara ya [[Ulaya]] na [[Asia]] pamoja na tako la bara baharini - ni bamba la kibara

Pitio la 18:16, 23 Novemba 2019

Mabamba gandunia ya dunia yetu

Bamba gandunia ni jina kwa vipande vinavyofanya sehemu ya nje ya dunia yetu. Sehemu hii ya nje huitwa ganda la dunia na chini yake kuna sehemu ya dunia ambayo ni joto kiasi ya kwamba miamba na elementi zote zinapatikana katika hali ya giligili yaani kuyeyushwa. Hii sehemu ya nje ya dunia si kipande kimoja bali kuna vipande mbalimbali kandokando vinavyoelea juu ya mata ya moto ndani yake. Unaweza kusoma zaidi katika makala kuhusu muundo wa dunia.

Gandunia[1] ni elimu kuhusu ganda la dunia. Hoja la sayansi kuhusu gandunia ni ya kwamba ganda la dunia limevunjika kwa vipande mbalimbali vinavyoitwa mabamba. Kila bamba lapakana na mabamba mengine. Mabamba yasukumwa na mikondo ya moto chini yao kama majani yanayokaa usoni wa maji inayoanza kuchemka katika sufuria. Hivyo kila bamba lina mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba mengine. Tetemeko la ardhi ni dalili ya kwamba mabamba yamesuguana na hivyo kusababisha mishtuko tunayojua kama tetemeko la ardhi.

Mabamba haya ni sehemu ya nje ya tabakamwamba (lithosferi). Tabaka hili limevunjika katika vipande vikubwa 7 na vingine vidogo vinavyoelea juu ya tabaka lenye hali ya kiowevu chenye mnato mzito.

Mabamba haya yote yameonekana kuwa na mwendo wa sentimita kadhaa (2 - 20 cm zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huu husababishwa na nguvu ya magma (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba haya.

Mabamba makuu ya dunia

Mabamba makubwa ya ganda la nje ya dunia ni:

Kati ya mabamba madogo ni:

Mwendo wa mabamba: jinsi Pangaea ilivyoachana na kutokea kwa bara za leo

Mwendo wa mabamba

Mwendo wa mabamba haya umesababisha kutokea na kuvunjika kwa mabara katika historia ya dunia yetu.

Wataalamu hufikiri ya kwamba dunia ilikuwa na bara kubwa moja tu (Pangaea) miaka milioni 300 - 150 iliyopita iliyovunjika katika vipande au mabamba mbalimbali.

Hata mabamba yaliyopo kwa sasa yanategemewa kuendelea kuhamahama, kuvunjika au kupotea kabisa.

Kwa mfano Afrika iko katika mwenendo wa kupasuliwa kwenye mstari wa Bonde la Ufa yaani Afrika ya Mashariki inaelekea kujitenga na sehemu nyingine ya bara ikiwa bamba la pekee. Penye Bonde la Ufa la sasa bahari itatandiwa baada ya miaka milioni 20.

Bara Hindi au bamba la Uhindi inaendelea kusukuma dhidi ya bamba la Asia na kujisukuma chini ya milima ya Himalaya - kuna uwezekano ya kwamba itaingia kabisa na kutoweka.

Makala hiyo kuhusu "Bamba la gandunia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

  1. neno gandunia si kawaida bado, tunafuata hapo kamusi ya KAST.