Mlangobahari wa Bering : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16: Mstari 16:
{{mbegu-jio}}
{{mbegu-jio}}


[[Jamii:Milangobahari ya Amerika|B]][[Jamii:Milangobahari ya Asia|B]]
[[Category:Milango ya Bahari|B]]
[[Category:Aktiki]]
[[Category:Aktiki]]
[[Jamii:Historia ya Amerika]]
[[Jamii:Historia ya Amerika]]

Pitio la 16:52, 7 Oktoba 2019

Mlango wa Bering unavyoonekana kutoka angani
Ramani ya mlango wa Bering

Mlango wa Bering (kwa Kirusi: Берингов пролив; kwa Kiingereza: Bering Strait) ni mlango wa bahari na mahali pa kukaribiana kati ya Alaska upande wa Amerika ya Kaskazini na Siberia upande wa Asia.

Mlango wa Bering una upana wa takriban kilomita 92 na kina cha mita 30 hadi 50 pekee. Unaunganisha bahari ya Aktiki na Pasifiki.

Jina limetokana na Vitus Bering aliyekuwa Mdenmark katika utumishi wa Urusi aliyevuka mlango huu mwaka 1728.

Kando ya mlango wa Bering pande zote mbili maeneo yana watu wachache kwa sababu ya mazingira ya baridi.

Kufuatana na nadharia za wataalamu wa historia hapa palikuwa mahali pa kuvuka kwa watu wa kwanza kutoka Asia kwenda Amerika. Inafikiriwa ya kwamba wakati wa Enzi ya Barafu miaka 10,000 iliyopita kiasi kikubwa cha maji duniani kilipatikana kwa umbo la barafu na hivyo kiasi cha maji kiowevu kilikuwa kidogo kuliko leo. Kwa sababu hiyo usawa wa bahari ulikuwa takriban mita 121 chini ya uwiano wa leo[1] na mlango wa Bering ulikuwa mkavu ukapitika kwa miguu. Hivyo watu waliingia kwa mara ya kwanza barani Amerika.

Tanbihi

  1. [http://earth.rice.edu/mtpe/cryo/cryosphere/topics/ice_age/ice_sea.html As ice sheets build up sea level drops, exposing continental shelves], Tovuti ya rice.edu, ilitazamiwa Februari 2017
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.