Uingereza : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 58: Mstari 58:
|}
|}


'''Uingereza''' (pia: '''Ingilandi''', '''England''') ni nchi kubwa ndani ya [[Ufalme wa Muungano]] yenye wakazi milioni 50 au 83% ya wakazi wa Ufalme wote na eneo lake ni theluthi mbili ya kisiwa cha [[Britania]].
'''Uingereza''' (pia: '''Ingilandi''' kutoka [[Kiingereza]]: '''England''') ni nchi kubwa ndani ya [[Ufalme wa Muungano]] yenye wakazi [[milioni]] 50 (83[[%]] ya wakazi wote wa Ufalme) na eneo lake ni takriban [[km²]] 130,000 ([[theluthi]] [[mbili]] za [[kisiwa]] cha [[Britania]]).


==Jina==
==Jina==
Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini hali halisi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi kwenye kusini ya kisiwa, na nje yake kuna nchi za [[Welisi]] (Wales, upande wa magharibi) na [[Uskoti]] (Scotland, upande wa kaskazini).
Katika [[lugha]] ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini kwa usahihi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi [[kusini]] mwa kisiwa, tofauti na nchi za [[Welisi]] (Wales, upande wa [[magharibi]]) na [[Uskoti]] (Scotland, upande wa [[kaskazini]]).


Asili ya jina la Kiswahili ni neno <big>إنجليزي</big> ''injilisi'' ''(matamshi ya Kimisri: ingilisi)''" katika lugha ya [[Kiarabu]]; Waarabu walisikia jina "inglish" wakirahisisha matamshi kuwa "inglis", wakaongeza sauti fupi kati ya "g" na "l" hivyo kufikia kwa "ingilis" ambako "i" ya pili ni fupi kiasi cha kusikia pia "e" na hivyo ilipokelewa na Waswahili. Kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r": ingelesi kuwa ingereza.
[[Asili]] ya [[jina]] la [[Kiswahili]] ni neno <big>إنجليزي</big> ''injilisi'' ''(matamshi ya Kimisri: ingilisi)''" katika lugha ya [[Kiarabu]]; [[Waarabu]] walisikia jina "inglish" wakirahisisha matamshi kuwa "inglis", wakaongeza [[sauti]] fupi kati ya "g" na "l", hivyo kufikia kwa "ingilis" ambako "i" ya pili ni fupi kiasi cha kusikia pia "e" na hivyo ilipokewa na [[Waswahili]]. Kwa namna ya [[Kibantu]] sauti ya "l" ikawa "r": ingelesi kuwa ingereza.


== Jiografia ==
== Jiografia ==
Mstari 69: Mstari 69:
Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambacho ndicho kisiwa kikubwa cha [[Ulaya]]. Inapakana na [[Welisi]] upande wa magharibi na [[Uskoti]] upande wa kaskazini.
Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambacho ndicho kisiwa kikubwa cha [[Ulaya]]. Inapakana na [[Welisi]] upande wa magharibi na [[Uskoti]] upande wa kaskazini.


Upande wa magharibi iko Bahari ya Eire, na ng'ambo yake kisiwa cha [[Eire]] (Ireland). Upande wa mashariki iko [[Bahari ya Kaskazini]], ng'ambo yake [[Denmark]], [[Ujerumani]] na [[Uholanzi]]; upande wa kusini uko [[Mfereji wa Kiingereza]] halafu kusini-magharibi [[Bahari Atlantiki]], ng'ambo yake [[Ufaransa]] na [[Ubelgiji]]. Tangu mwaka [[1994]] chini ya mfereji huo kuna njia ya reli kwa [[tobwe]] inayounganisha Uingereza na Ufaransa.
Upande wa magharibi iko [[Bahari ya Eire]], na ng'ambo yake kisiwa cha [[Eire]] (Ireland). Upande wa [[mashariki]] iko [[Bahari ya Kaskazini]], ng'ambo yake [[Denmark]], [[Ujerumani]] na [[Uholanzi]]; upande wa kusini uko [[Mfereji wa Kiingereza]] halafu kusini-magharibi [[Bahari Atlantiki]], ng'ambo yake [[Ufaransa]] na [[Ubelgiji]]. Tangu mwaka [[1994]] chini ya mfereji huo kuna njia ya [[reli]] kwa [[tobwe]] inayounganisha Uingereza na Ufaransa.


Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni [[Isle of Wight]] katika kusini. [[Pwani]] zake ni ndefu, hakuna mahali palipo mbali zaidi ya [[km]] 113 kutoka [[bahari]]ni.
Eneo la Uingereza ni takriban [[km²]] 130,000 na hivyo theluthi mbili za kisiwa cha Britania.


Sehemu kubwa ya nchi ni ama tambarare au vilima vidogo; mwinuko wa juu ni [[Scafell Pike]] yenye [[kimo]] cha [[mita]] 978. Kumbe [[milima]] mirefu ya Britania iko Welisi na Uskoti.
Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni [[Isle of Wight]] katika kusini. Pwani zake ni ndefu, hakuna mahali palipo mbali zaidi ya km 113 kutoka [[bahari]].

Sehemu kubwa ya nchi ni ama tambarare au vilima vidogo; mwinuko wa juu ni Scafell Pike yenye kimo cha mita 978. Milima mirefu ya Britania iko katika Welisi na Uskoti.


===Tabianchi===
===Tabianchi===
Tabianchi ya Uingereza inaathiriwa na mahali pake baharini inayopitiwa na [[Mkondo wa Ghuba]] na [[latitudo|latitudo ya kaskazini]]. Athari hizi zinaleta tabianchi fufutende ya kibahari; kwa wastani baridi haishuki chini ya 0 [[°C]] na joto halipandi juu ya 32 °C. Hata hivyo vipindi vya [[jeledi]] au joto kali zaidi vinaweza kutokea kwa siku kadhaa. Miezi ya baridi ni Januari na Februari. Julai kwa kawaida ni mwezi mwenyo joto zaidi. Hali ya hewa mara nyingi ni nyevunyevu na mvua inaweza kutokea mwaka wote. Vipindi vya mvua na jua hubadilishana haraka.
[[Tabianchi]] ya Uingereza inaathiriwa na mahali pake baharini inayopitiwa na [[Mkondo wa Ghuba]] na [[latitudo|latitudo ya kaskazini]]. Athari hizo zinaleta tabianchi fufutende ya kibahari; kwa [[wastani]] [[baridi]] haishuki chini ya 0 [[°C]] na [[joto]] halipandi juu ya 32 °C. Hata hivyo vipindi vya [[jeledi]] au [[joto]] kali zaidi vinaweza kutokea kwa [[siku]] kadhaa. Miezi ya baridi ni [[Januari]] na [[Februari]]. [[Julai]] kwa kawaida ni mwezi wenye joto zaidi. [[Hali ya hewa]] mara nyingi ni nyevunyevu na [[mvua]] inaweza kutokea mwaka wote. Vipindi vya mvua na [[jua]] hubadilishana haraka.


===Miji ya Uingereza===
===Miji ya Uingereza===
Mji Mkuu ni [[London]]. Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: [[London]] (wakazi 9,787,426), [[Manchester]] (2,553,379), [[Birmingham]] (pamoja na West Midlands 2,440,986), [[Leeds]] (pamoja na West Yorkshire 1,777,934), [[Sheffield]], [[Bradford]] na [[Liverpool]].
[[Mji mkuu]] ni [[London]]. Kati ya [[miji]] mikubwa ya Uingereza ni: [[London]] (wakazi 9,787,426), [[Manchester]] (2,553,379), [[Birmingham]] (pamoja na West Midlands 2,440,986), [[Leeds]] (pamoja na West Yorkshire 1,777,934), [[Sheffield]], [[Bradford]] na [[Liverpool]].


=== Mito ya Uingereza ===
=== Mito ya Uingereza ===
[[Picha:CanalettoSomersetHouseTerrace.jpg|thumb|left|320px|Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750]]
[[Picha:CanalettoSomersetHouseTerrace.jpg|thumb|left|320px|Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750]]
Kutokana na tabianchi yenye mvua ya kutosha kuna mito mingi nchini. Mito mirefu ni Thames (km 346) na Severn (km 350).
Kutokana na tabianchi yenye mvua ya kutosha kuna [[mito]] mingi nchini. Mito mirefu ni Thames (km 346) na Severn (km 350).
* [[Severn (mto)|Severn]] (mto mrefu wa [[Britania]])
* [[Severn (mto)|Severn]] (mto mrefu wa [[Britania]])
* [[Thames (mto)|Thames]] (mto mrefu katika Uingereza)
* [[Thames (mto)|Thames]] (mto mrefu katika Uingereza)
Mstari 100: Mstari 98:
=== Mikoa ya Uingereza ===
=== Mikoa ya Uingereza ===
{{main|Mikoa ya Uingereza}}
{{main|Mikoa ya Uingereza}}
Kihistoria Uingereza iligawiwa kwa kaunti (''counties'') na miji (''boroughs'').
Kihistoria Uingereza iligawiwa katika [[kaunti]] (''counties'') na miji (''boroughs'').


Nchi yote imegawiwa leo kwa mikoa (regions) 9. Mikoa kadhaa huwa na mamlaka fulani ya kiutawala, lakini si yote. Menginevyo utawala wa kieneo kunatokea hasa kwenye ngazi ya kaunti na halmashauri ndani ya kila mkoa.
Nchi yote imegawiwa leo katika [[mikoa]] (regions) 9. Mikoa kadhaa huwa na [[mamlaka]] fulani ya kiutawala, lakini si yote. Vinginevyo [[utawala]] wa kieneo kunatokea hasa kwenye ngazi ya kaunti na [[halmashauri]] ndani ya kila mkoa.
{{Uingerezamap|width={{{width|250}}}|float=left}}
{{Uingerezamap|width={{{width|250}}}|float=left}}


== Historia ==
== Historia ==
Uingereza ilikaliwa na makabila ya [[Wabritania]] wenye lugha za [[Kikelti]] na kuvamiwa na [[Dola la Roma]] katika [[karne ya pili]] [[BK]]. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi [[karne ya tano]] BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.
Uingereza ilikaliwa na [[makabila]] ya [[Wabritania]] wenye lugha za [[Kikelti]] na kuvamiwa na [[Dola la Roma]] katika [[karne ya 2]] [[BK]]. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi [[karne ya 5]] BK. Wakati ule [[Waroma wa Kale|Waroma]] walipaswa kuondoa [[wanajeshi]] wao kisiwani kwa ajili ya [[ulinzi]] wa nchi za [[bara]].


=== Uvamizi wa Waanglia-Saksoni ===
=== Uvamizi wa Waanglia-Saksoni ===
Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya [[Kigermanik]] walivamia kisiwa hasa [[Wasaksoni]], [[Waanglia]] na [[Wadenmark]]. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.
Katika [[karne za 5]] na [[Karne ya 6|6]] BK makabila ya [[Kigermanik]] walivamia kisiwa hasa [[Wasaksoni]], [[Waangli]] na [[Wadenmark]]. Walileta [[Lugha za Kigermanik|lugha zao za Kigermanik]] zilizochukua nafasi ya lugha ya [[Wabritania]].


Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au [[Cornwall]] au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza:Brittany; Kifaransa: Bretagne).
Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au [[Cornwall]] au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda [[Britania Ndogo]] (Kiingereza: Brittany; [[Kifaransa]]: Bretagne).


Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka [[937]] Mfalme [[Athelstan]] aliweza kuunganisha karibu eneo lote la Uingereza ya leo.
[[Karne]] zilizofuata kisiwa kiliona [[madola]] madogo na hali ya [[vita]]. [[Mwaka]] [[937]] [[Mfalme]] [[Athelstan]] aliweza kuunganisha karibu eneo lote la Uingereza ya leo.


=== Uvamizi wa Wanormani ===
=== Uvamizi wa Wanormani ===
Mwaka [[1066]] wanajeshi [[Wanormani]] kutoka kaskazini ya Ufaransa walivamia Uingereza na kuteka yote chini ya mtemi [[William Mshindi]]. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha [[Kiingereza]].
Mwaka [[1066]] wanajeshi [[Wanormani]] kutoka kaskazini mwa Ufaransa walivamia Uingereza na kuiteka yote chini ya mtemi [[William Mshindi]]. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha [[Kiingereza]].


=== Ufalme wa Muungano ===
=== Ufalme wa Muungano ===
Tangu mwaka [[1601]] mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka [[1707]]. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania. Tangu 1801 jina likawa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu [[1927]] Uingereza ni sehemu ya [[Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini]] (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).
Tangu mwaka [[1601]] mfalme [[James VI wa Uskoti]] alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka [[1707]]. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa [[Ufalme wa Muungano wa Britania]].
Tangu mwaka [[1801]] jina likawa [[Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire]] (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi [[1927]] wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata [[uhuru]] wake. Tangu hapo Uingereza ni sehemu ya [[Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini]] (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).


[[Picha:Liverpool skyline.jpg|thumb|330px|Mji wa Liverpool]]
[[Picha:Liverpool skyline.jpg|thumb|330px|Mji wa Liverpool]]

Pitio la 07:17, 31 Agosti 2019

England
Uingereza
English Flag English Coat of Arms
(Bendera ya Uingereza) (Nembo la Uingereza)
Wito (Kifaransa): Dieu et mon droit
("Mungu na haki yangu")
Uingereza katika Ulaya
Uingereza kwenye visiwa vya Britania
Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Muungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Eire (buluu) upande wa magharibi
Lugha Kiingereza
Mji Mkuu London
Mji Mkubwa London
Eneo
– jumla

130,395 km²
Wakazi

2004
–sensa ya 2001
– Msongamano wa watu

50.1 millioni [1]

49,138,831 [2]
377/km²

Umoja wa nchi yote 927 BK na mfalme
Athelstan
Dini rasmi Church of England (Anglikana)
Pesa Pound sterling (£) (GBP)
Masaa UTC / (GMT)
Summer: UTC +1 (BST)
Ua la Taifa Waridi ya Tudor (nyekundu, nyeupe)
Mtakatifu wa kitaifa Mt George

Uingereza (pia: Ingilandi kutoka Kiingereza: England) ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Muungano yenye wakazi milioni 50 (83% ya wakazi wote wa Ufalme) na eneo lake ni takriban km² 130,000 (theluthi mbili za kisiwa cha Britania).

Jina

Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa chote cha Britania. Lakini kwa usahihi "Uingereza" ni ile sehemu kubwa zaidi kusini mwa kisiwa, tofauti na nchi za Welisi (Wales, upande wa magharibi) na Uskoti (Scotland, upande wa kaskazini).

Asili ya jina la Kiswahili ni neno إنجليزي injilisi (matamshi ya Kimisri: ingilisi)" katika lugha ya Kiarabu; Waarabu walisikia jina "inglish" wakirahisisha matamshi kuwa "inglis", wakaongeza sauti fupi kati ya "g" na "l", hivyo kufikia kwa "ingilis" ambako "i" ya pili ni fupi kiasi cha kusikia pia "e" na hivyo ilipokewa na Waswahili. Kwa namna ya Kibantu sauti ya "l" ikawa "r": ingelesi kuwa ingereza.

Jiografia

Mazingira ya vilima vya Devon, kusini-magharibi ya Uingereza

Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambacho ndicho kisiwa kikubwa cha Ulaya. Inapakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini.

Upande wa magharibi iko Bahari ya Eire, na ng'ambo yake kisiwa cha Eire (Ireland). Upande wa mashariki iko Bahari ya Kaskazini, ng'ambo yake Denmark, Ujerumani na Uholanzi; upande wa kusini uko Mfereji wa Kiingereza halafu kusini-magharibi Bahari Atlantiki, ng'ambo yake Ufaransa na Ubelgiji. Tangu mwaka 1994 chini ya mfereji huo kuna njia ya reli kwa tobwe inayounganisha Uingereza na Ufaransa.

Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini. Pwani zake ni ndefu, hakuna mahali palipo mbali zaidi ya km 113 kutoka baharini.

Sehemu kubwa ya nchi ni ama tambarare au vilima vidogo; mwinuko wa juu ni Scafell Pike yenye kimo cha mita 978. Kumbe milima mirefu ya Britania iko Welisi na Uskoti.

Tabianchi

Tabianchi ya Uingereza inaathiriwa na mahali pake baharini inayopitiwa na Mkondo wa Ghuba na latitudo ya kaskazini. Athari hizo zinaleta tabianchi fufutende ya kibahari; kwa wastani baridi haishuki chini ya 0 °C na joto halipandi juu ya 32 °C. Hata hivyo vipindi vya jeledi au joto kali zaidi vinaweza kutokea kwa siku kadhaa. Miezi ya baridi ni Januari na Februari. Julai kwa kawaida ni mwezi wenye joto zaidi. Hali ya hewa mara nyingi ni nyevunyevu na mvua inaweza kutokea mwaka wote. Vipindi vya mvua na jua hubadilishana haraka.

Miji ya Uingereza

Mji mkuu ni London. Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: London (wakazi 9,787,426), Manchester (2,553,379), Birmingham (pamoja na West Midlands 2,440,986), Leeds (pamoja na West Yorkshire 1,777,934), Sheffield, Bradford na Liverpool.

Mito ya Uingereza

Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750

Kutokana na tabianchi yenye mvua ya kutosha kuna mito mingi nchini. Mito mirefu ni Thames (km 346) na Severn (km 350).

Mikoa ya Uingereza

Makala kuu: Mikoa ya Uingereza

Kihistoria Uingereza iligawiwa katika kaunti (counties) na miji (boroughs).

Nchi yote imegawiwa leo katika mikoa (regions) 9. Mikoa kadhaa huwa na mamlaka fulani ya kiutawala, lakini si yote. Vinginevyo utawala wa kieneo kunatokea hasa kwenye ngazi ya kaunti na halmashauri ndani ya kila mkoa.

Historia

Uingereza ilikaliwa na makabila ya Wabritania wenye lugha za Kikelti na kuvamiwa na Dola la Roma katika karne ya 2 BK. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi karne ya 5 BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.

Uvamizi wa Waanglia-Saksoni

Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya Kigermanik walivamia kisiwa hasa Wasaksoni, Waangli na Wadenmark. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.

Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza: Brittany; Kifaransa: Bretagne).

Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka 937 Mfalme Athelstan aliweza kuunganisha karibu eneo lote la Uingereza ya leo.

Uvamizi wa Wanormani

Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini mwa Ufaransa walivamia Uingereza na kuiteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.

Ufalme wa Muungano

Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na wafalme wa pamoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Muungano wa Britania.

Tangu mwaka 1801 jina likawa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu hapo Uingereza ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Mji wa Liverpool

Marejeo

  1. Office for National Statistics - UK population approaches 60 million
  2. Office for National Statistics - 2001 census Population profile - England.

Viungo vya nje