Machakos : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Adding: ca:Machakos
d roboti Nyongeza: nl:Machakos (stad), no:Machakos
Mstari 25: Mstari 25:
[[ca:Machakos]]
[[ca:Machakos]]
[[en:Machakos]]
[[en:Machakos]]
[[nl:Machakos (stad)]]
[[no:Machakos]]
[[sr:Махакос]]
[[sr:Махакос]]
[[sv:Machakos]]
[[sv:Machakos]]

Pitio la 00:57, 2 Februari 2008

Location of Machakos in Kenya
Location of Machakos in Kenya

Machakos ni mji wa Kenya katika Ukambani takriban kilomita 64 upande wa kusini-mashariki wa Nairobi. Ni makao makuu ya Wilaya ya Machakos na mji mkubwa wa Mkoa wa Mashariki.

Machakos imekua haraka kwa sababu ni karibu na mji mkuu wa taifa imeshapita idadi ya wakazi lakhi na nusu. Wenyeji wa Machakos ni hasa Wakamba.

Historia

Machakos ni kati ya miji ya kwanza ya Kenya bara ikaundwa mwaka 1899 wa Waingereza na kuwa makao makuu ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (mbali na eneo lindwa la pwani lililokodishwa na Usultani wa Zanzibar na Uingereza) kwa muda mfupi.

Jina la mji lilitokana na chifu Masaku wa Wakamba aliyewahi kuwa na boma lake hapo.

Baada ya azimio la kutounganisha Machakos na reli ya Uganda mji haukuendelea sana.

Mwaka 2002 majadiliano kati ya pande mbalimbali za vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudani yalifanyika Machakos.

Kituo kikuu cha mabasi mjini Nairobi huitwa na wenyeji "Machakos Airport".


Viungo vya Nje