Wapangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Wapangwa''' ni [[kabila]] la [[watu]] kutoka [[Milima Livingstone]] karibu na [[pwani]] ya [[mashariki]] ya [[Ziwa Nyasa]], [[wilaya ya Ludewa]], [[Mkoa wa Njombe]], [[kusini]] mwa nchi ya [[Tanzania]]. [[Mwaka]] [[2002]] [[idadi]] ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.
'''Wapangwa''' ni [[kabila]] la [[watu]] kutoka [[Milima Livingstone]] karibu na [[pwani]] ya [[mashariki]] ya [[Ziwa Nyasa]], [[wilaya ya Ludewa]], [[Mkoa wa Njombe]], [[kusini]] mwa nchi ya [[Tanzania]].
[[Mwaka]] [[2002]] [[idadi]] ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.


[[Lugha]] yao ni [[Kipangwa]].
[[Lugha]] yao ni [[Kipangwa]].


==Historia==
==Historia==
Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya [[Ludewa]] (Madunda, Mawengi, Mlangali, Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea [[Njombe]]. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni [[vita]], maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile Malawi na Msumbiji, kwa ajili ya vita.
Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya [[Ludewa]] (Madunda, Mawengi, Mlangali, Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea [[Njombe]]. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni [[vita]], maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile [[Malawi]] na [[Msumbiji]], kwa ajili ya vita.


==Uchumi==
==Uchumi==
Wapangwa hulima [[mazao]] mbalimbali ya [[chakula]] katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya [[mito]]. Hulima kwa [[ushirika]] unaoitwa njhiika. Pia hulima mazao ya [[biashara]] kama [[kahawa]], [[chai]], [[pareto]], [[mahindi]]. Kabila hili pia hupata [[matunda]] ya asili kama vile: masada, savula, makuhu, mahofita, mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.
Wapangwa hulima [[mazao]] mbalimbali ya [[chakula]] katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya [[mito]]. Hulima kwa [[ushirika]] unaoitwa njhiika. Pia hulima mazao ya [[biashara]] kama [[kahawa]], [[chai]], [[pareto]], [[mahindi]]. Kabila hili pia hupata [[matunda]] ya asili kama vile: masada, savula, makuhu, mahofita, mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.


Pia ni [[wafugaji]] wa makundi madogomadogo ya [[ng'ombe]], [[mbuzi]], [[kondoo]] na [[nguruwe]] ([[kitimoto]]). Tena Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na [[uwindaji]] wa [[wanyamapori]] kama vile (kwa lugha yao) nyhaluchi ,mahtu ngwehe, sudi, ng'ese, ng'wali ni videke.
Pia ni [[wafugaji]] wa [[makundi]] madogomadogo ya [[ng'ombe]], [[mbuzi]], [[kondoo]] na [[nguruwe]] ([[kitimoto]]). Tena Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na [[uwindaji]] wa [[wanyamapori]] kama vile (kwa lugha yao) nyhaluchi ,mahtu ngwehe, sudi, ng'ese, ng'wali ni videke.


==Utamaduni==
==Utamaduni==
Chakula chao ni [[ugali]] wa [[mahindi]], [[ulezi]] na [[mtama]] kidogo. [[Kitoweo]] cha vyakula hivyo ni [[maharage]], [[samaki]], [[nyama]] na jamii ya [[Mboga|mbogamboga]].
Chakula chao ni [[ugali]] wa [[mahindi]], [[ulezi]] na [[mtama]] kidogo. [[Kitoweo]] cha vyakula hivyo ni [[maharage]], [[samaki]], [[nyama]] na jamii ya [[Mboga|mbogamboga]].


Kinywaji chao ni [[pombe]] (ukhimbi) yaani kangala, komoni, [[ulanzi]] ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao [[mlanzi]]. Ulanzi ni pombe ya asili sana kwa Wapangwa, maana ni jadi kwao kunywa ulanzi, na hata watoto wadogo hupewa ulanzi kama juisi. Ulanzi, kwa Wapangwa ni pombe ambayo inaheshimika sana, maana hata wanapokwenda shambani, huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka mfanyakazi shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya kazi, mpaka apewe ulanzi.
[[Kinywaji]] chao ni [[pombe]] (ukhimbi) yaani kangala, komoni, [[ulanzi]] ambao hugemwa kutoka katika [[mmea]] uitwao [[mlanzi]]. Ulanzi ni pombe ya asili sana kwa Wapangwa, maana ni [[jadi]] kwao kunywa ulanzi, na hata [[watoto]] wadogo hupewa ulanzi kama [[juisi]]. Ulanzi, kwa Wapangwa ni pombe ambayo inaheshimika sana, maana hata wanapokwenda [[Shamba|shambani]], huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka [[mfanyakazi]] shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya [[kazi]], mpaka apewe ulanzi.


Hata katika harusi na sherehe nyingine za kimila kama vile kujengea [[Kaburi|makaburi]] (Mahoka), mila za kumrudisha mjane nyumbani (Ngotora), mila za kuabudu [[miungu]], n.k., ulanzi ndio huwa unatumika zaidi ya pombe nyingine.
Hata katika [[harusi]] na [[sherehe]] nyingine za kimila kama vile kujengea [[Kaburi|makaburi]] (Mahoka), [[mila]] za kumrudisha [[mjane]] nyumbani (Ngotora), mila za kuabudu [[miungu]], n.k., ulanzi ndio huwa unatumika zaidi ya pombe nyingine.


Kwa hiyo, Wapangwa wote (kama vile kina Willah, Haule, Muligo, Mtweve, Ngairo, Mwinuka n.k.), ambao bado wanatii mila na desturi zao, ulanzi kwao ni jadi.
Kwa hiyo, Wapangwa wote (kama vile kina Willah, Haule, Muligo, Mtweve, Ngairo, Mwinuka n.k.), ambao bado wanatii mila na [[desturi]] zao, ulanzi kwao ni jadi.
Usafiri wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.


[[Mavazi]] yao ya asili ni [[nguo]] zilizotengenezwa kwa [[ngozi]] za [[wanyama]] pamoja na magome ya [[miti]] ya misambi ambayo hupondwapondwa, hufumwa na kupakwa mono.
[[Mavazi]] yao ya asili ni [[nguo]] zilizotengenezwa kwa [[ngozi]] za [[wanyama]] pamoja na magome ya [[miti]] ya misambi ambayo hupondwapondwa, hufumwa na kupakwa mono.
Mstari 25: Mstari 26:
[[Nyumba]] zao kwa sasa ni za [[matofali]] ya [[udongo]] ya kuchoma na kuezekwa kwa [[bati]], hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti kugandikwa kwa [[udongo wa mfinyanzi]] na kuezekwa kwa [[nyasi]] aina ya hunji na lihanu.
[[Nyumba]] zao kwa sasa ni za [[matofali]] ya [[udongo]] ya kuchoma na kuezekwa kwa [[bati]], hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti kugandikwa kwa [[udongo wa mfinyanzi]] na kuezekwa kwa [[nyasi]] aina ya hunji na lihanu.


[[Usafiri]] wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.
== Viungo vya Nje ==

[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]
== Viungo vya nje ==
* [http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]


{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
Mstari 32: Mstari 35:
{{Makabila ya Tanzania}}
{{Makabila ya Tanzania}}
[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]
[[Jamii:Wilaya ya Ludewa]]

Pitio la 12:33, 13 Agosti 2019

Wapangwa ni kabila la watu kutoka Milima Livingstone karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, kusini mwa nchi ya Tanzania.

Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.

Lugha yao ni Kipangwa.

Historia

Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya Ludewa (Madunda, Mawengi, Mlangali, Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea Njombe. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni vita, maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile Malawi na Msumbiji, kwa ajili ya vita.

Uchumi

Wapangwa hulima mazao mbalimbali ya chakula katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito. Hulima kwa ushirika unaoitwa njhiika. Pia hulima mazao ya biashara kama kahawa, chai, pareto, mahindi. Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile: masada, savula, makuhu, mahofita, mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.

Pia ni wafugaji wa makundi madogomadogo ya ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe (kitimoto). Tena Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na uwindaji wa wanyamapori kama vile (kwa lugha yao) nyhaluchi ,mahtu ngwehe, sudi, ng'ese, ng'wali ni videke.

Utamaduni

Chakula chao ni ugali wa mahindi, ulezi na mtama kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni maharage, samaki, nyama na jamii ya mbogamboga.

Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, ulanzi ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi. Ulanzi ni pombe ya asili sana kwa Wapangwa, maana ni jadi kwao kunywa ulanzi, na hata watoto wadogo hupewa ulanzi kama juisi. Ulanzi, kwa Wapangwa ni pombe ambayo inaheshimika sana, maana hata wanapokwenda shambani, huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka mfanyakazi shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya kazi, mpaka apewe ulanzi.

Hata katika harusi na sherehe nyingine za kimila kama vile kujengea makaburi (Mahoka), mila za kumrudisha mjane nyumbani (Ngotora), mila za kuabudu miungu, n.k., ulanzi ndio huwa unatumika zaidi ya pombe nyingine.

Kwa hiyo, Wapangwa wote (kama vile kina Willah, Haule, Muligo, Mtweve, Ngairo, Mwinuka n.k.), ambao bado wanatii mila na desturi zao, ulanzi kwao ni jadi.

Mavazi yao ya asili ni nguo zilizotengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa, hufumwa na kupakwa mono.

Nyumba zao kwa sasa ni za matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati, hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu.

Usafiri wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wapangwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.