Jerry Rawlings : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 75: Mstari 75:
Wazazi wake wanaitwa Victoria Agbotui na James Ramsey John.  Mama yake alitoka Gold Coast.  Baba yake aliishi katika ngome ya Douglas katika Kirkcudbrightshire nchi ya Scotland.  Makabila ya mama yake yalikuwa Nzema na Ewe lakini hii haikuathiri siasa zake.  

== Elimu na hudumu kwa jeshi ==
== Elimu na huduma kwa jeshi ==
Alienda shule ya upili ya Achimota kisha alisoma Chuo cha Achimota.  Alijunga na Jeshi la Anga la Ghana muda mfupi baadaye.  Katika Jeshi la Anga, aliishi Takoradi, katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana, ili kuendelea na masomo.  Yeye alihitimu mnamo mwezi wa kwanza mwaka 1969 na kuwa Afisa Mwanahewa. Yeye alikuwa luteni katika jeshi la anga la Ghana mwezi wa nne mwaka wa 1978.

Pitio la 16:17, 28 Julai 2019

Rais wa Ghana (1st President of the 4th Republic)
In office7 January 1993 – 7 January 2001
Vice President Kow Nkensen Arkaah (1993–1997)John Atta Mills (1997–2001)
Preceded by Himself
Succeeded by John Agyekum Kufuor
Head of State of Ghana
In office31 December 1981 – 7 January 1993
Vice President None
Preceded by Hilla Limann
Head of State of Ghana
In office4 June 1979 – 24 September 1979
Preceded by General Fred Akuffo
Succeeded by Hilla Limann
Personal details
Born 22 June 1947 (age 72)Accra, Gold Coast (now Ghana)
Political party military – AFRC (1979)military – PNDC (1981–93)Multi-Party Democracy – NDC(1993–2001)
Spouse(s) Nana Konadu Agyeman Rawlings
Children 5
Profession Fighter pilot
Awards UDS Honorary Award
Military service
Allegiance Ghana
Branch/service Ghana Air Force
Years of service 1968–92
Rank Flight Lieutenant

Jerry Rawlings (alizaliwa Accra, koloni la Gold Coast, 22 Juni 1947) ni rais wa zamani wa Ghana na afisa wa zamani wa kijeshi. Aliongoza nchi ya Ghana kutoka mwaka wa 1981 hadi mwaka wa 2001 na kwa muda mfupi mwaka wa 1979. Pamoja na viongozi wengine wa kijeshi, walitawala mpaka mwaka wa 1992. Baadaye, Mzee Rawlings aliunda National Democratic Congress (NDC) na aliwahi kuwa rais wa Ghana mara mbili.

Maisha ya utotoni

Wazazi wake wanaitwa Victoria Agbotui na James Ramsey John.  Mama yake alitoka Gold Coast.  Baba yake aliishi katika ngome ya Douglas katika Kirkcudbrightshire nchi ya Scotland.  Makabila ya mama yake yalikuwa Nzema na Ewe lakini hii haikuathiri siasa zake.  

Elimu na huduma kwa jeshi

Alienda shule ya upili ya Achimota kisha alisoma Chuo cha Achimota.  Alijunga na Jeshi la Anga la Ghana muda mfupi baadaye.  Katika Jeshi la Anga, aliishi Takoradi, katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana, ili kuendelea na masomo.  Yeye alihitimu mnamo mwezi wa kwanza mwaka 1969 na kuwa Afisa Mwanahewa. Yeye alikuwa luteni katika jeshi la anga la Ghana mwezi wa nne mwaka wa 1978.

Mzee Rawlings aliongoza vita mbili za mapinduzi katika mwaka wa 1979 dhidi ya Ignatius Kutu Acheampong na Jenerali Fred Akuffo na mwaka wa 1981 dhidi ya Rais Hilla Limann. Mzee Rawlings hakufurahishwa na serikali ya Ignatius Kutu Acheampong ambaye alipindua serikali nyingine na  kuanza uongozi mwezi wa kwanza mwaka wa 1972. Rawlings hakumpenda Acheampong kwa sababu alishutumiwa kwa ufisadi na kuifanya nchi ya Ghana kutegemea mifumo ya serikali ya kabla ya ukoloni.  Hii ilisababisha kuporomoka kwa uchumi na kuongezeka kwa viwango vya umaskini.

Mnamo tarehe 15 mwezi wa tano mwaka wa 1979, wiki tano kabla ya uchaguzi wa kitaifa, Rawlings na askari wengine sita walifanya mapinduzi dhidi ya serikali ya Jenerali Acheampong, lakini walishindwa na alikamatwa na Jeshi la Ghana.  Alihukumiwa hadharani kifo.  Wakati wakingojea kuuawa kwake, Rawlings alitoroka kutoka kizuizini tarehe 4 mwezi wa sita mwaka wa 1979 na kikundi cha askari.  Mnamo mwaka wa 1982 alijaribu mapinduzi mengine dhidi ya Rais Hilla Limann na akafanikiwa.  Mzee Rawlings alitawala kupitia Provisional National Defence Council (PNDC) hadi mwaka wa 1992.  Kisha akawania urais na akashinda.

Familia

Yeye alifunga ndoa na Nana Konadu Agyeman.  Walikutana katika chuo Kikuu cha Achimota.  Wana watoto wanne.  Wana watoto watatu wa kike wanaitwa Ezanetor Rawlings, Yaa Asantewaa, na Amina Rawlings.  Wana mtoto mmoja wa kiume anaitwa Kimith Rawlings.  

Maisha ya baada ya urais

Mnamo mwezi wa kumi na moja mwaka wa 2000, Mzee Rawlings alipewa tuzo ya kwanza ya Year of Volunteers 2001 Eminent Person na katibu wa Umoja wa Mataifa.  Baada ya kupokea tuzo, alizungumza kuhusu kujitolea.  Mnamo mwezi wa kumi mwaka wa 2010, yeye alikuwa mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika nchini Somalia. Sasa yeye hutoa hotuba katika vyuo vikuu.

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jerry Rawlings kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.