Nzi (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6: Mstari 6:


==Jina==
==Jina==
Nzi ni kati ya kundinyota zilizobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka Dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Haikujulikani kwa Wagiriki wa Kale au Waarabu waliojifunza kutoka kwao. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi [[Pieter Dirkszoon Keyser]] na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea [[Indonesia]] zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika [[globu ya nyota]] ya [[Petrus Plancius]].
Nzi ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka Dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Haikujulikani kwa Wagiriki wa Kale au Waarabu waliojifunza kutoka kwao. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi [[Pieter Dirkszoon Keyser]] na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea [[Indonesia]] zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika [[globu ya nyota]] ya [[Petrus Plancius]].


Keyser alitumia jina la [[Kiholanzi]] De Vlieghe ([[Nzi]]) lililotajwa baadaye kwa jina la ''Kilatini'' "Musca“. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya [[Johann Bayer]] aliyetumia njia ya "Apis" (nyuki) na hivyo kuna vitabu vya zamani vinavyotumia jina Apis lakini baadaye "Musca" ilirudishwa.
Keyser alitumia jina la [[Kiholanzi]] De Vlieghe ([[Nzi]]) lililotajwa baadaye kwa jina la ''Kilatini'' "Musca“. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya [[Johann Bayer]] aliyetumia njia ya "Apis" (nyuki) na hivyo kuna vitabu vya zamani vinavyotumia jina Apis lakini baadaye "Musca" ilirudishwa.

Pitio la 12:27, 20 Julai 2019

Nyota za kundinyota Nzi (Musca) katika sehemu yao ya angani

Nzi (kwa Kilatini na Kiingereza Musca) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.

Mahali pake

Nzi iko jirani na kundinyota mashuhuri ya Salibu (Crux) iliyopo upande wa kaskazini, Mkuku (en:Carina) upande wa magharibi, Kinyonga (Chamaeleon) upande wa kusini , Ndege wa Peponi (Apus) na Bikari (Circinus) upande wa kaskazini-mashariki.

Jina

Nzi ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka Dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Haikujulikani kwa Wagiriki wa Kale au Waarabu waliojifunza kutoka kwao. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius.

Keyser alitumia jina la Kiholanzi De Vlieghe (Nzi) lililotajwa baadaye kwa jina la Kilatini "Musca“. Baadaye ilipokelewa katika "Uranometria" ya Johann Bayer aliyetumia njia ya "Apis" (nyuki) na hivyo kuna vitabu vya zamani vinavyotumia jina Apis lakini baadaye "Musca" ilirudishwa.

Leo Musca ipo pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2] Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Mus'.[3]

Nyota

Nyota angavu zaidi ni α Alfa Muscae yenye mwangaza unaoonekana wa 2.7 mag ikiwa umbali wa Dunia wa miakanuru 310[4] Ni rahisi kuiona maana ni nyota angavu jirani na Salibu kwa kufuata mstari wa urefu wa Salibu kuelekea kusini.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Musca" katika lugha ya Kilatini ni "Muscae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Muscae, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  4. Alphamus (Alpha Muscae), tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje

Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano