Basi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
No edit summary
d Protected "Basi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho))
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:43, 19 Julai 2019

Basi dogo huko Novoaltaisk.
Basi la safari ndefu huko Krakow, Polandi.
Flixbus huko Ujerumani.

Basi (kutoka Kiingereza "bus") ni motokaa kubwa inayotumika kusafirisha watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Mabasi hutofautishwa kutokana na matumizi hasa kutokana na umbali wa safari.

  • mabasi ya safari za karibu hutumiwa mjini na pia kati ya vijiji au miji ya karibu. Mara nyingi hufuata ratiba maalumu. Katika miji mikubwa hufuatana kila baada ya dakika kadhaa. Ndani ya miji ambako hayana mwendo wa kasi kubwa kuna nafasi kwa abiria wanaosimama, lakini kwa kawaida abiria huketi.
    • kwa usafiri wa mjini penye idadi kubwa wa abiria kuna mabasi yenye ghorofa la juu, pia mabasi marefu yenye sehemu mbili zinazounganishwa kwa kiungo.
    • mabasi ya usafiri wa mjini hayainuliwa sana juu ya uwiano wa barabara ili abiria waweze kushuka na kuingia haraka
  • mabasi ya safari za mbali hayabebi idadi kubwa ya abiria kama mabasi ya mjini. Hapa kwa kawaida viti ni vizuri zaidi ili abiria waone raha kwenye safari ya masaa mengi.
    • Kuna mabasi yenye choo ndani yake.
    • mabasi ya safari za mbali huinuliwa juu zaidi kwa sababu abiria hufika na mizigo yao inayopakizwa kwenye sehemu ya chini; sehemu ya abiria iko juu ya tabaka penye mizigo, injini na tangi ya mafuta.
    • Mabasi ya safari za mbali huwa pia na chumba cha kulala cha dereva wa pili maana madereva wa mabasi huwa na masharti kuhusu idadi ya masaa ambayo hayaruhusiwi kupita kwa sababu za usalama.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.