Jicho : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 3: Mstari 3:
'''Jicho''' ni sehemu ya [[mwili]] inayowezesha kuona. Ni [[ogani]] inayotambua [[mwanga]] na kutuma habari zake kwa [[ubongo]].
'''Jicho''' ni sehemu ya [[mwili]] inayowezesha kuona. Ni [[ogani]] inayotambua [[mwanga]] na kutuma habari zake kwa [[ubongo]].


Macho Ndicho Chombo Pekee Kinacholeta Furaha Katika Mwili Mzima.
== Aina za macho ya viumbehai ==
Kuna mifumo mbalimbali ya macho kati ya aina mbalimbali za [[wanyama]].

Macho ya kimsingi kwa [[viumbehai]] vidogo yanatambua tu kama [[mazingira |mazingira]] yana mwanga au la. Hata kati ya viumbehai wenye [[seli]] moja kuna wenye [[protini]] zinazotofautisha [[giza]] na [[nuru]]. Kuna [[konokono]] ambao hawawezi "kuona" [[picha]] ya mazingira lakini wanatambua mwanga na uwezo huu unawawezesha kuepukana na mwanga wa [[jua]] ambao ungewakausha.

Macho yaliyoendelea kiasi yana [[umbo]] kama [[kikombe]] na hii inawezesha kutambua upande gani nuru inatokea.

[[Wanyama]] wengi huwa na macho yaliyoendelea zaidi: yana uwezo wa kuona picha halisi ya mazingira pamoja na [[rangi]] na [[mwendo]].
[[Picha:Drosophilidae_compound_eye.jpg|thumb||Jicho la nzi (drosophila) chini ya [[hadubini]]; [[lenzi]] ya kila [[omatidi]] inaonekana kama [[nusu tufe]].]]


== Macho ya kuungwa ==
== Macho ya kuungwa ==

Pitio la 05:48, 30 Juni 2019

Jicho la binadamu
Macho ya kuungwa ya nzi

Jicho ni sehemu ya mwili inayowezesha kuona. Ni ogani inayotambua mwanga na kutuma habari zake kwa ubongo.

Macho Ndicho Chombo Pekee Kinacholeta Furaha Katika Mwili Mzima.

Macho ya kuungwa

Wadudu na arthropoda huwa na macho ya kuungwa na vijicho vingi vidogo vinavyoitwa omatidi; kila kijicho huwa na umbo la kijiti na kwenye mwisho wake kuna lenzi ya chitini. Mdudu anaweza kuwa na vijicho elfu kadhaa na picha ya mazingira inaunganishwa na picha nyingi ndogo za kila kijicho.

Macho haya ya kuungwa yanamwezesha mdudu kuangalia asilimia kubwa ya mazingira yake: kwa aina kadhaa hata nyuma yake. Macho ya kuungwa yanaweza kufunika hadi asilimia 80 ya eneo la kichwa. Mdudu haoni vikali kama mtu lakini anaona mabadiliko na mwendo haraka sana.

Wanyama wanaoishi katika vilindi vya bahari penye giza nene huwa na macho ambamo fuwele ziko kama kioo na kupazia nuru hafifu.

Kuna wanyama wanaoweza kuona nuru ambayo ni nje ya upeo wa kibinadamu; kwa mfano nyuki huona mnururisho wa infraredi.

Macho ya mamalia

Macho ya binadamu kama ya mamalia huwa na lenzi moja tu. Lakini muundo wa jicho unaruhusu kuona rangi, umbali na mengi madogo.

Shida za macho

Shida za macho ni nyingi kama vile upofu, kutoona rangi, macho kujiliza, wekundu uliokithiri pamoja na kutoa majimaji. Shida hizo huletwa na vumbi, kuzaliwa ukiwa kipofu, jua jingi bila kuvalia miwani vizuia jua.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jicho kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.