Marangu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|Lango la kuingia Kilimanjaro National Park. File:Marangu waterfalls.jpg|thumb|Maporomoko ya Maji ya M...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:04, 26 Juni 2019

Lango la kuingia Kilimanjaro National Park.
Maporomoko ya Maji ya Marangu.

Marangu ni mji ulioko katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Historia

Kabla ya uhuru mwaka 1961, mji wa Marangu ulikuwa ni makao makuu ya wilaya ya Vunjoiliyokuwa chini ya (Mangi Mwitori) Petro Itosi Marealle na (Mangi Mkuu) Thomas Marealle, aliyepewa ufalme mwaka 1951, ambaye aliishi katika mji wa Mosh. Neno "Marangu" linamaanisha mahali penye vijiti vingi vya maji. Mji huu ni kati ya maeneo maarufu nchini Tanzania.

Uchumi

Wakazi wengi wa Marangu ni wakulima wa ndizi, mboga za majani na kahawa. Hata hivyo, chanzo kikuu cha mapato ni utalii kutokana na Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine.

Elimu

Shule mbalimbali na vyuo, kama vile Chuo cha Ualimu cha Marangu na Shule ya Washichana ya Ashira, ziko katika mji huu zikitoa huduma kwa wanafunzi toka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Tazama pia