Batiki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ' thumb|upright|200px|Batiki ya Indonesia '''Batiki''' ni ufundi wa u...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 03:17, 26 Juni 2019

Batiki ya Indonesia

Batiki ni ufundi wa uchapaji urembo kwenye nguo kwa kutumia rangi na nta wenye asili ya Indonesia. [1] Batiki hutokana na kuchorwa kwa matone na miistari kwa kutumia nyenzo iitwayo tjanting au kwa kutumia nyenzo ya shaba iitwayo cap.[n 1][2]

Desturi ya kutengeneza nguo za batiki ipo katika nchi mbalimbali ila Indonesia ndio nchi inayojulikana zaidi kwa desturi hii.[3][4]

Ingawa batiki inatengenezwa kwenye miji mbalimbali huko Indoesia[5], batiki ya kisiwa cha Java ndio inayoaminika kuwa ya ustadi wa juu kabisa duniani. Oktoba 2009, UNESCO iliitambua batiki ya Indonesia kuwa Masterpiece of Oral and Intangible Heritage of Humanity.[6]

Neno batik linatokana na lugha ya Kijava. Huenda limetokana na neno la Kijava amba ('kuandika') na titik ('kitone'), au limetokana na neno lenye asili ya Proto-Austronesia *beCík ('kuchora mwilini'). Neno hili lilitokea kwa mara ya kwanza kwenye Kamusi Elezo ya Britannica mwaka 1880, ambapo liliandikwa battik. Wakati wa ukoloni wa Uholanzi maneno yaliyotumika ni pamoja na: mbatek, mbatik, batek and batik.[7][8][9]

Marejeo

  1. "What is Batik?". The Batik Guild. 
  2. The Jakarta Post Life team. "Batik: a cultural dilemma of infatuation and appreciation", The Jakarta Post. 
  3. Robert Pore (12 February 2017). "A unique style, Hastings artist captures wonder of crane migration". The Independent.  Check date values in: |date= (help)
  4. Sucheta Rawal (4 October 2016). "The Many Faces of Sustainable Tourism - My Week in Bali". Huffingtonpost.  Check date values in: |date= (help)
  5. "Handwriting Batik (Batik Tulis) And Cities In Indonesia That Produce It". Iliwekwa mnamo June 26, 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. ""Indonesian Batik", Inscribed in 2009 on the Representative List of the Intangible Cultural Heritage of Humanity". UNESCO. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 October 2014. Iliwekwa mnamo 10 October 2014.  Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  7. Oxford English Dictionary: Batik
  8. Dictionary.com: Batik
  9. Blust, Robert (Winter 1989). "Austronesian Etymologies - IV". Oceanic Linguistics 28 (2): 111–180. JSTOR 3623057. doi:10.2307/3623057.  Check date values in: |date= (help)


Viungo vya nje

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Hitilafu ya kutaja: <ref> tags exist for a group named "n", but no corresponding <references group="n"/> tag was found