Yosia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 17: Mstari 17:


==Familia==
==Familia==
Mwana wa mfalme [[Amon]] na [[Jedidah]]<ref name=je>[http://www.jewishencyclopedia.com/articles/8926-josiah "Josiah", ''Jewish Encyclopedia'']</ref>, Yosia alirithi utawala akiwa [[mtoto]] wa miaka 8 tu, kutokana na [[uuaji]] wa [[baba]] yake, akatawala miaka 31,<ref>[[2Fal]] 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26</ref> kuanzia 641/[[640 KK]] hadi [[610 KK]]/609 KK.<ref>Edwin Thiele, ''[[The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings]]'', (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.</ref>
Mwana wa [[mfalme Amon]] na [[Jedidah]]<ref name=je>[http://www.jewishencyclopedia.com/articles/8926-josiah "Josiah", ''Jewish Encyclopedia'']</ref>, Yosia alirithi utawala akiwa [[mtoto]] wa miaka 8 tu, kutokana na [[uuaji]] wa [[baba]] yake, akatawala miaka 31,<ref>[[2Fal]] 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26</ref> kuanzia 641/[[640 KK]] hadi [[610 KK]]/609 KK.<ref>Edwin Thiele, ''[[The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings]]'', (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.</ref>


Anatajwa pia katika [[Injili ya Mathayo]] kama [[babu]] wa [[Yesu]].
Anatajwa pia katika [[Injili ya Mathayo]] kama [[babu]] wa [[Yesu]].
Mstari 31: Mstari 31:
==Urekebisho==
==Urekebisho==
[[File:Close-Up.jpg|thumb|right|220px|Ua wa ndani wa [[Hekalu la Solomoni]].]]
[[File:Close-Up.jpg|thumb|right|220px|Ua wa ndani wa [[Hekalu la Solomoni]].]]
Kwa miaka 13 tu ([[622 K.K.|622]] - [[609 K.K.]]) [[Yosia]] alifanya urekebisho wa kidini kuanzia [[Yerusalemu]] hadi kwa mabaki ya [[Waisraeli]] wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu [[sadaka]] nje ya [[hekalu la Yerusalemu]].
Kwa miaka 13 tu ([[622 K.K.|622]] - [[609 K.K.]]) Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia [[Yerusalemu]] hadi kwa mabaki ya [[Waisraeli]] wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu [[sadaka]] nje ya [[hekalu la Yerusalemu]].


Kipindi hicho [[mji mkuu]] wa [[Ashuru]] uliangamizwa alivyotabiri kwa [[furaha]] [[nabii Nahumu]] ([[612 KK|612]] hivi K.K.).
Kipindi hicho [[mji mkuu]] wa [[Ashuru]] uliangamizwa alivyotabiri kwa [[furaha]] [[nabii Nahumu]] ([[612 KK|612]] hivi K.K.).
Mstari 44: Mstari 44:
*Hertz J.H. (1936) The Pentateuch and Haftoras. Deuteronomy. Oxford University Press, London.
*Hertz J.H. (1936) The Pentateuch and Haftoras. Deuteronomy. Oxford University Press, London.
*[[Richard Elliott Friedman|Friedman, R.]] (1987) Who wrote the Bible? New York: Summit Books
*[[Richard Elliott Friedman|Friedman, R.]] (1987) Who wrote the Bible? New York: Summit Books

==Viungo vya nje==
==Viungo vya nje==
*[http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=564&letter=J&search=Josiah Jewish Encyclopedia: Josiah]
*[http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=564&letter=J&search=Josiah Jewish Encyclopedia: Josiah]

Pitio la 14:46, 29 Mei 2019

Mfalme Yosia katika ibada hekaluni

Yosia, kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake "aliyeponywa na YHWH" au "aliyetegemezwa na Yah"[1][2]; kwa Kigiriki Ιωσιας; kwa Kilatini Josias; (649 KK609 KK) alikuwa mfalme wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika wakati huo.

Hasa alitumia nguvu zake zote kutekeleza agizo la gombo lililopatikana mwaka 622 KK likidai sadaka zote zitolewe katika hekalu la Yerusalemu tu, kadiri ya msimamo wa Kumbukumbu la Torati: "Mungu mmoja, hekalu moja".

Ndiyo maana Biblia inamsifu kwa namna ya pekee pamoja na Hezekia kati ya wafalme wote wa Israeli na Yuda, mbali na Daudi aliyebaki kielelezo cha kudumu cha mtawala aliyempeneza Mungu.

Familia

Mwana wa mfalme Amon na Jedidah[3], Yosia alirithi utawala akiwa mtoto wa miaka 8 tu, kutokana na uuaji wa baba yake, akatawala miaka 31,[4] kuanzia 641/640 KK hadi 610 KK/609 KK.[5]

Anatajwa pia katika Injili ya Mathayo kama babu wa Yesu.

Lakini nje ya Biblia hatajwi popote.[6]

Babu yake, Manase anatajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kwa jinsi alivyoelekeza raia zake kuacha ibada ya Mungu mmoja ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu, kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia.

Yosia alizaa watoto wa kiume wanne: Yohane, Eliakimu[7], Matania na Shalumu.[8]

Kwanza Shalumu alimrithi Yosia kwa jina la Yehoahazi.[9] lakini baada ya miezi tu nafasi yake ilishikwa na Eliakimu kwa jina la Yehoyakimu,[10] halafu na mtoto wa huyo, Yekonia;[11] hatimaye alitawala Matania kwa jina la Sedekia.[12] Huyo akawa mfalme wa mwisho wa Yuda kwa kushindwa na Babuloni aliyoisaliti, akapelekwa uhamishoni huko pamoja na Wayahudi wengi mwaka 586 KK.

Urekebisho

Ua wa ndani wa Hekalu la Solomoni.

Kwa miaka 13 tu (622 - 609 K.K.) Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya Waisraeli wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu sadaka nje ya hekalu la Yerusalemu.

Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha nabii Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini Yosia alipokufa vitani kabla ya wakati mambo yakaharibika haraka sana, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na juhudi zake binafsi, mbali ya kuungwa mkono na watu wachache kama nabii Yeremia.

Tanbihi

  1. Josiah definition - Bible Dictionary - Dictionary.com. Retrieved 25 July 2011.
  2. Wells, John C. (1990). Longman pronunciation dictionary. Harlow, England: Longman. uk. 386. ISBN 0-582-05383-8.  entry "Josiah"
  3. "Josiah", Jewish Encyclopedia
  4. 2Fal 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26
  5. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.
  6. Alpert, Bernard; Alpert, Fran (2012). Archaeology and the Biblical Record. Hamilton Books. uk. 74. ISBN 978-0761858355. 
  7. 2 Kings 23:34
  8. 1Nya 3:15; 2Fal 23:36; 2Fal 24:18; 2Fal 23:31
  9. 1Nya 3:15; Yer 22:11
  10. 2Nya 36:4;
  11. 2Nya 36:8
  12. 2Fal 24:17

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.