Kalenga : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Kalenga ''' ni [[jina]] la [[kata]] ya [[Wilaya ya Iringa Vijijini]] katika [[Mkoa wa Iringa]], [[Tanzania]] yenye [[Postikodi Tanzania|Postikodi namba]] 51201. Kwa mujibu wa [[sensa]] iliyofanyika mwaka wa [[2012]], kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,963 waishio humo.<ref>[http://www.wavuti.weebly.com/uploads/3/0/7/6/3076464/census20general20report20-202920march202013_combined_final20for20printing1.pdf Sensa ya 2012, Iringa Region- Iringa District Council]</ref> [[Msimbo wa posta]] ni 51201.

Hadi mwanzo wa ukoloni Kalenga ilitwa pia "Iringa"; baada ya Wajerumani kuanzisha "Iringa Mpya" kwenye mahali pa mji wa leo waliita mahali asilia "Iringa ya Kale".

==Kalenga na historia ya mtemi Mkwawa==
==Kalenga na historia ya mtemi Mkwawa==
[[Picha:Skull of Mkwawa.jpg|thumb|320px|[[Fuvu la kichwa]] cha Mtemi Mkwawa katika makumbusho ya Kalenga.]]
[[Picha:Skull of Mkwawa.jpg|thumb|320px|[[Fuvu la kichwa]] cha Mtemi Mkwawa katika makumbusho ya Kalenga.]]

Pitio la 08:32, 18 Mei 2019

Kalenga ni jina la kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51201. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,963 waishio humo.[1] Msimbo wa posta ni 51201.

Hadi mwanzo wa ukoloni Kalenga ilitwa pia "Iringa"; baada ya Wajerumani kuanzisha "Iringa Mpya" kwenye mahali pa mji wa leo waliita mahali asilia "Iringa ya Kale".

Kalenga na historia ya mtemi Mkwawa

Fuvu la kichwa cha Mtemi Mkwawa katika makumbusho ya Kalenga.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal

Kalenga ilikuwa makao makuu ya Mtemi Mkwawa[2] aliyeongoza upinzani wa Wahehe dhidi ya ukoloni wa Kijerumani katika miaka ya 1891 - 1896. Huko Kalenga Mkwawa aliwahi kujenga boma imara ya mawe baada ya kujifunza kuhusu uenezaji wa Wajerumani kutoka sehemu za pwani. Boma hii liliitwa Lipuli. Ujenzi ulianza mnamo 1887 ukachukua miaka minne.

Baada ya kushindwa kwa jeshi la Schutztruppe la Kijerumani katika mapigano ya Lugalo mwaka 1891, Wajerumani walirudi kwa nguvu zaidi wakashambulia Lipuli - Kalenga kwenye Oktoba 1894 kwa silaha kali kama mizinga na bombomu.

Mkwawa alifaulu kukimbia wakati wa kutekwa kwa boma. Akaendelea kuendesha vita ya msituni hadi kujiua mwaka 1898 alipoona hatari ya kukamatwa ilhali alijeruhiwa vibaya. Inasemekana Wajerumani walikata kichwa chake na kutuma fuvu Ujerumani.

Baada ya kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, washindi, hasa Uingereza, walisisitiza fuvu lirudishwe: hivyo kuna fungu 246 katika Mkataba wa Versailles linalotaja fuvu la Mkwawa. Wajerumani walidai baadaye wanashindwa kulikuta, hivyo ilichelewa hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati jeshi la Uingereza lilikuwa na utawala juu ya sehemu za Ujerumani ya kwamba Waingereza waliteua fuvu moja katika mkusanyiko wa Makumbusho ya Bremen na kulituma Tanganyika kama fuvu la Mkwawa.

Kalenga kuna makumbusho kwa heshima ya Mtemi Mkwawa na fuvu hilo linahifadhiwa humo tangu kurudishwa mwaka 1954.

Marejeo

Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kalenga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.