Mhindi (kundinyota) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
<sup>Kwa maana tofauti ya jina hili tazama [[Muhindi]] na [[Uhindi]]</sup>
<sup>Kwa maana tofauti ya jina hili tazama [[Muhindi]] na [[Uhindi]]</sup>
[[Image: Mhindi Indus.png |thumb|right|400px|Nyota za kundinyota Mhindi (Indus) katika sehemu yao ya angani]]
[[Image: Mhindi Indus.png |thumb|right|390px|Nyota za kundinyota Mhindi (Indus) katika sehemu yao ya angani]]
'''Mhindi''' (kwa [[Kilatini]] na [[Kiingereza]] ''[[:en:Indus (constellation)|Indus]]'') <ref>[[Uhusika milikishi]] ''([[:en:genitive]])'' ya neno "Indus" katika lugha ya [[Kilatini]] ni "Indi" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Indi, nk.</ref> ni [[jina]] la [[kundinyota]] linaloonekana katika [[angakusi]] ya [[Dunia]] yetu.
'''Mhindi''' (kwa [[Kilatini]] na [[Kiingereza]] ''[[:en:Indus (constellation)|Indus]]'') <ref>[[Uhusika milikishi]] ''([[:en:genitive]])'' ya neno "Indus" katika lugha ya [[Kilatini]] ni "Indi" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Indi, nk.</ref> ni [[jina]] la [[kundinyota]] linaloonekana katika [[angakusi]] ya [[Dunia]] yetu.


Mstari 7: Mstari 7:


==Jina==
==Jina==
Mhindi linapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Hazikutajwa katika vitabu vya Wagiriki wa Kale au Waarabu. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi [[Pieter Dirkszoon Keyser]] na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea [[Indonesia]] zikaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika [[globu ya nyota]] ya [[Petrus Plancius]] na kupokelewa katika “Uranometria” ya [[Johann Bayer]]..
Mhindi inapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Nyingi hazikutajwa katika vitabu vya Wagiriki wa Kale au Waarabu. Kundinyota hili lilibuniwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi [[Pieter Dirkszoon Keyser]] na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea [[Indonesia]] likaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika [[globu ya nyota]] ya [[Petrus Plancius]] na kupokelewa katika “Uranometria” ya [[Johann Bayer]].


Keyser alitumia jina la [[Kiholanzi]] “De Indiaen” (yaani Mhindi) lililotajwa baadaye kwa jina la [[Kilatini]] „Indus“. Jina hili alilitumia kama kumbukumbu ya watu aliowaona mara ya kwanza katika maisha yake kwenye eneo la Bahari ya Hindi pale Madagaska na kwenye visiwa vya Indonesia. Baadaye alichukuliwa mara kadhaa kwa maana ya “Wahindi Wekundu” yaani Maindio wa Marekani ambayo si maana ya kiasili.
Keyser alitumia jina la [[Kiholanzi]] “De Indiaen” (yaani Mhindi) lililotajwa baadaye kwa jina la [[Kilatini]] „Indus“. Jina hili alilitumia kama kumbukumbu ya watu aliowaona mara ya kwanza katika maisha yake kwenye eneo la Bahari ya Hindi pale Madagaska na kwenye visiwa vya Indonesia. Baadaye alichukuliwa mara kadhaa kwa maana ya “Wahindi Wekundu” yaani Maindio wa Marekani ambayo si maana ya kiasili.
Mstari 14: Mstari 14:


==Nyota==
==Nyota==
Mhindi haina nayota angavu sana. Nyota angavu zaidi ni α Alfa Indi yenye [[uangavu unaoonekana|mwangaza unaoonekana]] wa [[mag]] 3.1 ikiwa na umbali kutuka duniani wa Dunia wa [[miaka ya nuru|miakanuru]] 101<ref>[ http://stars.astro.illinois.edu/sow/persian.html The Persian (Alpha Indi)], tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017; Kaler anatumia kwa nyota hii jina la Kichina “The Persian” isiyo kawaida</ref>. Beta Indi ina mag 3.7 ipo kwa umbali wa miakanuru 600 kutoka kwetu. Delta Indi ina mag 4.4 na ipo umbali wa miakanuru 185.
Mhindi haina nayota angavu sana. Nyota angavu zaidi ni α Alfa Indi yenye [[uangavu unaoonekana|mwangaza unaoonekana]] wa [[mag]] 3.1 ikiwa umbali kutoka Dunia wa [[miaka ya nuru|miakanuru]] 101<ref>[ http://stars.astro.illinois.edu/sow/persian.html The Persian (Alpha Indi)], tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017; Kaler anatumia kwa nyota hii jina la Kichina “The Persian” isiyo kawaida</ref>. Beta Indi ina mag 3.7 ipo kwa umbali wa miakanuru 600 kutoka kwetu. Delta Indi ina mag 4.4 na ipo umbali wa miakanuru 185.


Epsilon Indi yenye mag 4.69 ni kati ya nyota zilizo karibu sana na Dunia ikiwa na umbali wa miakanuru 11.8.
Epsilon Indi yenye mag 4.69 ni kati ya nyota zilizo karibu sana na Dunia ikiwa na umbali wa miakanuru 11.8.

Pitio la 19:33, 3 Mei 2019

Kwa maana tofauti ya jina hili tazama Muhindi na Uhindi

Nyota za kundinyota Mhindi (Indus) katika sehemu yao ya angani

Mhindi (kwa Kilatini na Kiingereza Indus) [1] ni jina la kundinyota linaloonekana katika angakusi ya Dunia yetu.

Mahali pake

Mhindi inapatikana kati ya nyota angavu za Alnair (α Alfa Gruis) katika Kuruki na Peacock (α Alfa Pavi) katika Tausi. Linapakana na makundinyota ya Kuruki (Grus) na Hadubini ( Microscopium) upande wa kaskazini, Darubini (en: Telescopium) na Tausi (Pavo) upande wa mashariki, Thumni (Octans) upande wa kusini na Tukani (Tucana) upande wa magharibi.

Jina

Mhindi inapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote katika karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Nyingi hazikutajwa katika vitabu vya Wagiriki wa Kale au Waarabu. Kundinyota hili lilibuniwa mara ya kwanza na mabaharia Waholanzi Pieter Dirkszoon Keyser na Frederick de Houtman katika safari yao ya kuelekea Indonesia likaonyeshwa mara ya kwanza mwaka 1598 katika globu ya nyota ya Petrus Plancius na kupokelewa katika “Uranometria” ya Johann Bayer.

Keyser alitumia jina la Kiholanzi “De Indiaen” (yaani Mhindi) lililotajwa baadaye kwa jina la Kilatini „Indus“. Jina hili alilitumia kama kumbukumbu ya watu aliowaona mara ya kwanza katika maisha yake kwenye eneo la Bahari ya Hindi pale Madagaska na kwenye visiwa vya Indonesia. Baadaye alichukuliwa mara kadhaa kwa maana ya “Wahindi Wekundu” yaani Maindio wa Marekani ambayo si maana ya kiasili.

Leo Mhindi ipo pia katika orodha ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [2]. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Ind'.[3]

Nyota

Mhindi haina nayota angavu sana. Nyota angavu zaidi ni α Alfa Indi yenye mwangaza unaoonekana wa mag 3.1 ikiwa umbali kutoka Dunia wa miakanuru 101[4]. Beta Indi ina mag 3.7 ipo kwa umbali wa miakanuru 600 kutoka kwetu. Delta Indi ina mag 4.4 na ipo umbali wa miakanuru 185.

Epsilon Indi yenye mag 4.69 ni kati ya nyota zilizo karibu sana na Dunia ikiwa na umbali wa miakanuru 11.8.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Indus" katika lugha ya Kilatini ni "Indi" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Indi, nk.
  2. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  3. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  4. [ http://stars.astro.illinois.edu/sow/persian.html The Persian (Alpha Indi)], tovuti ya Prof. Jim Kaler, university of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017; Kaler anatumia kwa nyota hii jina la Kichina “The Persian” isiyo kawaida

Viungo vya Nje

Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano