Kimondo cha Mbozi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Protected "Kimondo cha Mbozi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho))
No edit summary
Mstari 9: Mstari 9:


Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za [[kasoko]]; kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa [[pembe butu]] sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na [[mmomonyoko]].
Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za [[kasoko]]; kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa [[pembe butu]] sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na [[mmomonyoko]].

==Tanbihi==
<references/>


==Viungo vya Nje==
==Viungo vya Nje==

Pitio la 08:41, 3 Mei 2019

Kimondo cha Mbozi

Coordinates: 9°06′28″S 33°02′14″E / 9.10778°S 33.03722°E / -9.10778; 33.03722

Kimondo cha Mbozi[1] ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa tkriban tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri 0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.[2]

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.

Tanbihi

  1. Wakati mwingine kinatajwa kama "Mbosi meteorite" kwa kufuata tahajia ya Kijerumani ya jina la Mbozi
  2. [https://onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1111/j.1945-5100.1996.tb02036.x Edward J. OLSEN, Robert N. CLAYTON, Toshiko K. MAYEDA, Andrew M. DAVIS, Roy S. CLARKE Jr., John T. WASSON; Mbosi: An anomalous iron with unique silicate inclusions], jarida la Meteoritics & Planetary Science, Volume31, Issue5, September 1996

Viungo vya Nje

Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano