Kimondo cha Mbozi : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
d Protected "Kimondo cha Mbozi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho)) |
(Hakuna tofauti)
|
Pitio la 08:38, 3 Mei 2019
Coordinates: 9°06′28″S 33°02′14″E / 9.10778°S 33.03722°E
Kimondo cha Mbozi[1] ni kimondo ambacho kimeanguka kutoka angani karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa tkriban tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania.
Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.
Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8,69%, sulfuri 0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.[2]
Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.