KwaZulu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 17 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q594798 (translate me)
Mstari 1: Mstari 1:
[[Image:KwaZulu.png|right|thumb|Maeneo ya KwaZulu]]
[[Image:KwaZulu in South Africa.svg|right|thumb|Maeneo ya KwaZulu]]
[[Image:KwaZulu flag 1985.svg|thumb|200px|Bendera ya KwaZulu 1985-1994]]
[[Image:KwaZulu flag 1985.svg|thumb|200px|Bendera ya KwaZulu 1985-1994]]
[[Image:KwaZulu flag 1977.svg|thumb|200px|Bendera ya KwaZulu 1977-1985]]
[[Image:KwaZulu flag 1977.svg|thumb|200px|Bendera ya KwaZulu 1977-1985]]

Pitio la 01:12, 1 Mei 2019

Maeneo ya KwaZulu
Bendera ya KwaZulu 1985-1994
Bendera ya KwaZulu 1977-1985

KwaZulu ilikuwa bantustan katika Afrika Kusini wakati wa siasa ya apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). Iliundwa na serikali ya Afrika Kusini kama eneo kwa ajili ya Wazulu.

Mji mkuu ulikuwa mwanzoni Nongoma na tangu 1980 Ulundi.

Kiongozi wa KwaZulu hadi kufutwa kwa eneo mwaka 1994 alikuwa chifu Mangosuthu Buthelezi aliyeongoza chama cha Inkatha Freedom Party.

Buthelezi alikataa kukubali hali ya kujitawala kwa KwaZulu kama mabantustan mengine yaliyotangazwa kuwa nchi za pekee nje ya Afrika Kusini hata kama uhuru huu ulikuwepo tangazo tu lisilokubaliwa na jumuiya ya kimataifa. Hata hivyo mwaka 1977 KwaZulu ilipata kiwango cha kujitawala kama eneo chini ya Afrika Kusini.

Bantustan ilifutwa mwaka 1994 na kuunganishwa na jimbo la awali la Natal kuwa jimbo jipya la KwaZulu-Natal.