Ufalme wa Muungano : Tofauti kati ya masahihisho

Majiranukta: 55°N 3°W / 55°N 3°W / 55; -3
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 61: Mstari 61:
==GDP==
==GDP==


'''2.8 Trillioni Dollars {{Increase}}'''
'''2.92 Trillioni Dollars {{Increase}}'''


==Historia==
==Historia==

Pitio la 16:39, 21 Machi 2019

Ufalme wa Muungano


Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (kwa Kiingereza: United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland); kifupi "Ufalme wa Muungano" (Kiing.: United Kingdom) ni nchi ya visiwani ya Ulaya ya kaskazini-magharibi.

Mara nyingi huitwa kwa Kiswahili "Uingereza" tu ingawa nchi ya Uingereza ni moja tu kati ya sehemu za ufalme huo pamoja na Uskoti, Welisi na Eire ya Kaskazini.

Nchi iliongoza mapinduzi ya viwanda duniani, ilienea katika mabara yote kwa makoloni yake mengi ikabaki hadi leo kati ya nchi muhimu zaidi ulimwenguni.

Ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Mataifa, ambapo ana kiti cha kudumu na kura ya turufu katika Halmashauri ya Usalama, pia ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ingawa inajiandaa kujitoa.

GDP

2.92 Trillioni Dollars increase

Historia

Milki kubwa kwenye kisiwa cha Britania ilikuwa Uingereza.

Tangu mwaka 1284 Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Hati ya Muungano (Act of Union) ya mwaka 1536 ilikuwa sehemu ya Milki ya Uingereza.

Hati ya Muungano ya mwaka 1707 iliunganisha milki mbili za Uingereza na Uskoti kuwa Milki ya Britania Kuu. Nchi zote mbili zilikuwa chini ya mfalme mmoja tangu mwaka 1603. Tangu wakati uleule Ufalme wa Eire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia.

Sheria ya mwaka 1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).

Baada ya Vita vya uhuru vya Eire bunge la London kwa sheria ya mwaka 1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.

Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka 1922 uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu 1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.

Mwaka 1999 Uskoti, Welisi na Northern Ireland zilirudishwa mabunge yao ya pekee.

Uskoti ulikuwa na harakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Muungano lakini katika kura ya watu wa Uskoti ya mwaka 2014 asilimia 55 waliamua kubaki.

Kumbe kura ya wananchi wa Ufalme mzima ya mwaka 2016 iliamua kuondoka katika Umoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9.

Wakazi

Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2011, 59.5% za wakazi ni Wakristo (hasa wa Anglikana, halafu Wakatoliki, Wakalvini na wengineo), 4.4% ni Waislamu, 1.3% ni Mabanyani. 25.7% hawana dini yoyote.

Muungano na utawala

Bendera Nchi Hali Wakazi Vitengo Mji mkuu
Uingereza Ufalme 50,431,700

Mikoa
Wilaya

London
Uskoti Ufalme 5,094,800

Wilaya

Edinburgh
Welisi Utemi 2,958,600

Wilaya

Cardiff
Hapana Eire ya Kaskazini Jimbo 1,724,400

Wilaya

Belfast

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Serikali
Taarifa za jumla
Safari

55°N 3°W / 55°N 3°W / 55; -3

Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufalme wa Muungano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.