Mpanda (mji) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d wikidata interwiki
Mstari 15: Mstari 15:
[[Jamii: Miji ya Tanzania]]
[[Jamii: Miji ya Tanzania]]
[[Jamii:Wilaya ya Mpanda mjini|*]]
[[Jamii:Wilaya ya Mpanda mjini|*]]


[[en:Mpanda]]

Pitio la 15:02, 18 Machi 2019

Mpanda ni makao makuu na pia mji mkubwa wa Mkoa wa Katavi katika magharibi ya Tanzania. Ni kitovu muhimu cha biashara ya mazao kama mahindi na mpunga kuna pia dalili ya uchumi wa madini hasa dhahabu katika mazingira yake.

Mji umekua sana kuanzia wakazi 46,000 mwaka 2002 hadi kufikia idadi ya wakazi 102,000 wakati wa sensa ya 2012. [1]

Hadi mwaka 2014 hapakuwa na barabara za lami bali njia za udongo pekee hivyo usafiri huwa na shida wakati wa mvua. Kuna njia ya reli kutoka hapa hadi Kaliua inapoungana na Reli ya Kati. Safari ya reli hadi Tabora inachukua masaa 10 - 12. Mabasi yanaenda kila siku Sumbawanga (masaa 5), Mbeya na Tabora (masaa 9). Tangu kuwa makao makuu ya mkoa wa Katavi uwanja wa ndege uliboreshwa mwaka 2012.

Upande wa dini kuna makao makuu ya dayosisi wa Kikatoliki pamoja na dayosisi ya Anglika ya Ziwa Rukwa na makanisa ya Moravian, AIC, Assemblies na pia msikiti mbalimbali.

Marejeo

Kigezo:Kata za Wilaya ya Wilaya ya Mpanda Mjini