Njia Nyeupe : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 5: Mstari 5:
Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona [[galaksi]] yetu ambamo [[mfumo wa jua|mfumo wa Jua letu]] pamoja na Dunia ni sehemu yake.
Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona [[galaksi]] yetu ambamo [[mfumo wa jua|mfumo wa Jua letu]] pamoja na Dunia ni sehemu yake.


Galaksi yetu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Inafanana na kisahani chenye [[umbo]] la [[parafujo]]. [[Kipenyo]] cha kisahani hicho ni [[miaka ya nuru]] 100,000 ikiwa na [[unene]] wa miaka ya nuru 3,000.
Galaksi yetu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Inafanana na kisahani chenye [[umbo]] la [[parafujo]]. [[Kipenyo]] cha kisahani hicho ni [[miakanuru]] 100,000 ikiwa na [[unene]] wa miaka ya nuru 3,000.


Galaksi iliyo karibu zaidi angani inaitwa [[galaksi ya Andromeda|Andromeda]] ikiwa na [[umbali]] wa miaka ya nuru [[milioni]] 2.5.
Galaksi iliyo karibu zaidi angani inaitwa [[galaksi ya Andromeda|Andromeda]] ikiwa na [[umbali]] wa miaka ya nuru [[milioni]] 2.5.

Pitio la 15:38, 13 Machi 2019

Njia nyeupe jinsi inavyoonekana usiku (Mistari mekundu inaonyesha mipaka yake; sehemu ya chini imefichwa na mti)
Galaksi yetu jinsi inaaminiwa kuonekana vile kama tunaiangalia kutoka juu; picha ya galaksi ya mbali yenye mikono miwili ya parafujo

Njia Nyeupe (kwa Kiingereza Milky Way), pia majarra au "mkokoto wa kondoo za Sumaili" [1] ni jina la mlia mpana wa nyota nyingi unaoonekana angani wakati wa usiku kama wingu jeupe linalong`aa.

Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona galaksi yetu ambamo mfumo wa Jua letu pamoja na Dunia ni sehemu yake.

Galaksi yetu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Inafanana na kisahani chenye umbo la parafujo. Kipenyo cha kisahani hicho ni miakanuru 100,000 ikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000.

Galaksi iliyo karibu zaidi angani inaitwa Andromeda ikiwa na umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5.

Isipokuwa sayari za jua letu na kometi (zinazoonekana mara chache tu) na galaksi ya Andromeda (inayoonekana kama nyota 1), nyota zote ni kama jua letu.

Kuonekana kwa Njia Nyeupe kutoka duniani

Nyota karibu zote tunazoziona kwa macho yetu wakati wa usiku ni sehemu za Njia Nyeupe. Wakati wa giza tunaweza kuona kati ya nyota 3,000 hadi 5,000 bila msaada wa darubini.

Si rahisi kuona nyota nyingi tukiwa mjini, kwenye taa nyingi wakati wa usiku, kwa sababu mwanga wa taa za mjini unaakisiwa katika angahewa na kuzuia kuona mwanga kutoka nje ya angahewa.

Idadi kubwa zaidi ya nyota za Njia Nyeupe hatuwezi kuona wala kubainisha, kwa hiyo zinatokea machoni kama ukungu mweupe tu.

Uwezo wetu wa kuona nyota nyingi umepunguzwa na kuwepo kwa mavumbi ya kinyota kati ya mahali petu na kitovu cha galaksi.

Muundo

Galaksi yetu ina umbo la parafujo (spirali) ya kisahani. Mahali petu pamoja na jua pako kando kiasi ndani ya uwiano wa kisahani hiki. Tuko takriban 2/3 ya umbali wa kipenyo kutoka kitovu cha kisahani.

Ikitazamwa kutoka juu galaksi yetu ina umbo la parafujo lenye mikono mbalimbali. Picha hii tumeipata kutokana na kuangalia galaksi za mbali angani zinazoonekana kutoka juu na parafujo inaonekana.

Marejeo

  1. Yaani njia ya kondoo wa Ismaili; kuhusu majina ya nyota na sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina asilia linganisha Jan Knappert, The Cosmology of Swahili Islamic Literature, in: Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch [1]

Soma pia

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Njia Nyeupe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano