Binadamu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Bongo Ume Tajwa Kwa Ku Vumbua
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 74: Mstari 74:
* [[Mtu wa kwanza alitoka wapi]]
* [[Mtu wa kwanza alitoka wapi]]


Kama Munao Ufwata Wimbo Wa King Of Josue Discover Nani Ata Utolea?
==Tanbihi==
{{marejeo}}


==Viungo vya nje==
==Viungo vya nje==

Pitio la 07:13, 15 Desemba 2018

Binadamu
Homo sapiens sapiens
Homo sapiens sapiens
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Familia ya juu: Hominoidea (Wanyama kama binadamu)
Familia: Hominidae (Walio na mnasaba na binadamu)
Nusufamilia: Homininae (Wanaofanana sana na binadamu)
Jenasi: Homo
Linnaeus, 1758
Spishi: H. sapiens
Linnaeus, 1758
Nususpishi: H. s. sapiens
Mchoro wa uenezi wa jenasi Homo katika miaka milioni mbili ya mwisho. Rangi ya samawati Inaonyesha uwepo wa spishi fulani wakati na mahali fulani.[1]

Binadamu (pia mwanadamu) ni neno linalomaanisha "Mwana wa Adamu", anayeaminiwa na dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza.

Binadamu kadiri ya sayansi

Kisayansi jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya Homo sapiens ili kumtofautisha na viumbe wengine wa jenasi Homo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.

Watu wote walioko leo hii ni spishi ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile yao katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu.

Utafiti juu ya DNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo Afrika walau miaka 250,000 hivi iliyopita.

Kwa namna ya pekee, upimaji wa DNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, ulionyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita.

Halafu upimaji wa kromosomu Y, ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, ulionyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya baadhi ya watu kuanza kuhama bara la Afrika na kuenea Asia labda kufuatia pwani za Bahari ya Hindi.

Hata hivyo, miaka hii ya mwisho imegundulika katika baadhi ya wanaume wenye asili ya makabila ya Wabangwa na Wambo (Camerun, Afrika ya Kati) aina ya kromosomu Y tofauti sana na ile ya wanaume wengine wote waliowahi kupimwa, kiasi cha kukadiria imetofautiana miaka 350,000 hivi iliyopita.

Vilevile, upimaji wa DNA ya mstari kwa jumla umeonyesha uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio wa kusini kwa Sahara, wana asilimia 1-6 ya urithi wa kibiolojia kutoka kwa aina nyingine za homo, hususan Homo neanderthalensis, ile ya pango la Denisova na ile iliyorithiwa na baadhi ya watu wa visiwa vya Andaman (India).

Kama hao waliweza kweli kuzaliana na Homo sapiens maana yake walikuwa spishi moja na yeye. Hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko miaka 200,000 iliyofikiriwa kwanza.

Uenezi wa binadamu

Kutoka bara la Asia, watu walienea kwanza Australia na Ulaya, halafu Amerika toka kaskazini hadi kusini.

Hatimaye, katika karne ya 20 watu walikwenda kukaa kwa muda katika bara la Antaktika kwa ajili ya utafiti.

King of Josue Discover alizaliwa Katika Mwaka wa 2002 huko #Rutshuru, #Muramb, Jimbo Kivu ya Kaskazini, mwa, Kongo Ya Kidemocratia. Alikuwa Muimbaji wenye hana Timu lolote Ama (musicien Of-non group). Alizaliwa: 16 Décemba. Mwaka. Wa 2002.

UPINZANI WAKE KWENYE VITU VYAKE

=>2016: Huyo King of Josue Discover anapanga kujitowelea jina akijita "KJD"

=>2017: Watu Wengi Waja Kwake Wa kimpigia Kelele ehe: Sasa Sisi hatuja fahamishwa Kama iyo Jina Husema Nini: Tafa dhali Nao Tuna Omba Utupe msemwa Huo Unao Jita Eti Wewe Ni "kJd#

=>2018: Mwaka huu wa 2018 ndio aliwa Zungu Muzia Watu Wale na Kuwa Jibu: Mimi Na Jiita 'KJD' na nina Jua Kama Jina hio Kusema Nini Ndo Mana Yake na Jiita. Mimi Ninayo Siri Kwenye Jina Langu. Kwenye Jina hiyo husema "KJD" ndio manayake hii: "King of Josue Discover" na Mwenyi Husema eti Siya Uona Mkubwa ama Babu na Wa #Roi. Mimi niko Pahali Pale. Na Bongo Sibongo lime Tetwa Popote. Mimi Nipo Popote Na Udogo Wangu Wakati Nilipo Mdogo: Ukweli Upate Hapo:http://m.facebook.com/Kjd.Discover

Mimi Mwenyewe Na Ji Tetea Kwanza: Sifatani Na Bina Damu Husudi Hawaja Nipa Kitu.

Binadamu na elimunafsia

Karne XX imeleta maendeleo makubwa katika elimunafsia (= saikolojia). Hivyo anaweza kutambua vizuri mema na mabaya yaliyomo ndani mwake.

Lakini akitaka kujifahamu haitoshi asikilize mafundisho hayo au kusoma vitabu vingi juu yake.

Anahitaji kuishi katika mazingira bora ambapo ajisikie nyumbani, huru na mtulivu kwa kupendana na wenzake, kusikiliza watu wanaomfahamu (hasa walezi wake) wanasema nini juu yake, kujipatia muda wa kutulia peke yake na kujifikiria kulingana na maneno yao, kujichunguza kwa makini kuanzia miaka ya utotoni.

Kwa kuwa utu unategemea urithi, mazingira na utashi wa kila mmoja, anapaswa kuchunguza hayo yote yaliyochangia kumjenga.

Mara kwa mara ajitenge na watu na shughuli ili kutathmini tena maisha yake, kupima maono yake na kuweka maazimio ya kufaa, bila ya kusahau kwamba uhai wake ni fumbo, kwa kuwa unamtegemea Mungu.

Tazama pia

Kama Munao Ufwata Wimbo Wa King Of Josue Discover Nani Ata Utolea?

Viungo vya nje

  1. Stringer, C. (2012). "What makes a modern human". Nature 485 (7396): 33–35. PMID 22552077. doi:10.1038/485033a.