Tofauti kati ya marekesbisho "Wambunga"

Jump to navigation Jump to search
24 bytes added ,  miaka 2 iliyopita
no edit summary
 
==Historia==
Wambunga ni kabila dogo lililotokana na [[Wangoni]] baada ya mfarakano wa viongozi wa makundi yao walioingia katika eneo la [[Tanzania]] ya leo. Hivyo basi Wambunga ni Wangoni maseko (mafiti) walioingia [[Tanganyika]] kupitia [[kusini]] [[mashariki]] mwa [[Ruvuma]] wakiongozwa na [[kiongozi]] wa Wangoni maseko[[Maseko Mputa]].
 
Baada ya kutoelewana miongoni mwa makundi ya Wangoni kukapelekea [[chuki]] iliyosababisha viongozi wa makundi hayo kuuana wenyewe kwa wenyewe. Hivyo Mputa akauawa, na [[Mwana|mwanae]] Malunda akawa [[mtawala]] wa kundi hilo. Baadaye Malunda akawa na wasiwasi wa [[maisha]] yake kutokana na hali hiyo, hivyo akaamua kurudi na [[kundi]] la Wangoni masekoMaseko katika [[Zimbabwe]] ya leo walikotokea awali.
 
Lakini katika hilo baadhi yao waligoma kurudi Zimbabwe, ndipo baada ya Malunda kuondoka waliobaki wakahama pale [[Songea]] na kusogea [[mlima Mbunga]] ulioko pembezoni mwa [[mkoa wa Ruvuma]]. Baadaye, walipoona makundi ya Wangoni wakiendelea kupigana wao kwa wao, wakaamua kuondoka hapo [[mlima]] Mbunga na kuambaambaa [[Wilaya ya Ulanga|Ulanga]] (leo katika [[mkoa wa Morogoro]]), hasa kwenye [[bonde]] la [[mto Kilombero]].
 
Walijulikana kwa [[matamshi]] yao kuwa Wangoni, lakini wao walijiita Wambunga kwani wametokea mlima Mbunga. Hiyo ilitokana na kuchoshwa na [[vita]], maana wote waliwatambua Wangoni kwa kupenda vita, kumbe kwa kusema hivyo wangebaki salama wenyeji wao wasiwadhuru, maana wakati huo Wangoni walishaanza uchokozi wa kivita na [[MuyugumbaMunyigumba]], kiongozi wa [[Wahehe]].
 
Kwa sasa Wambunga wanapatikana zaidi katika maeneo yafuatayo: Ifakara mjini na vitongoji vyake, [[Kiberege]] na vitongoji vyake, [[Kisawasawa]], baadhi ya maeneo ya [[Mang'ula]], [[Mbingu (Kilombero)|Mbingu]] na baadhi ya maeneo ya [[Mngeta]]: maeneo yote haya ni katika wilaya ya Kilombero. Wambunga wapo kwa wingi katika [[kijiji]] cha [[Kisaki]], [[Wilaya ya Morogoro Vijijini|Morogoro vijijini]], mkoani Morogoro. Pia wanapatikana katika [[wilaya ya Kisarawe]], [[mkoa wa Pwani]]. Inasemekana baadhi ya Wambunga wapo katika maeneo ya nje ya [[Dar es Salaam]].

Urambazaji